Muonekano
wa Patchou Mwamba ‘Tajiri’ baada ya kupata uvimbe usoni.
Stori:
Erick Evarist
Vunja ukimya! Mwanamuziki mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo anayeitumikia Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ya Bongo, Patchou
Mwamba ‘Tajiri’ ameibuka na kufungukia skendo ya kufumaniwa iliyosambaa kwa
kasi kama moto wa kifuu, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo kamili.
Wikiendi
iliyopita, uvumi wa Patchou kufumaniwa uliibuka na kusambaa mitandaoni kufuatia
kuwepo kwa picha iliyomuonesha akiwa amevimba usoni hususan katika maeneo ya
macho na mdomoni.
Watu mbalimbali mitandaoni, walitumiana picha hiyo huku wakisindikiza na ujumbe
wa mtu aliyeiposti awali na kuandika kuwa mwanamuziki huyo amevimba baada ya
kufumaniwa na kutembezewa kichapo cha mbwa mwitu.
Wakati
Ijumaa Wikienda likiwa katika harakati ya kuchimba ukweli wa jambo hilo
(kawaida ya Global Publishers), mwanamuziki huyo alitinga katika ofisi za
gazeti hili na kutumia dakika 30 kuanika ukweli kuhusiana na uvumi huo.
“Nimesikitishwa
sana na jambo hili. Sijafumaniwa chochote, watu tu wameamua kunichafua. Mimi
nina ‘aleji’ na pombe, kuna dawa nilishauriwa niwe nakunywa kila ninapotaka
kunywa pombe.
|
No comments:
Post a Comment