|
Feisal
mtoto wa kwanza wa Aisha Madinda.
Kinachoshukiwa:
Marafiki wa
Aisha Madinda ambao nao ni waathirika wa madawa ya kulevya, wanadai Aisha
Madinda alirudia utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo wana mashaka kuwa
alitumia kiasi kikubwa kuliko inavyohitajika na pengine ndio sababu ya kifo
chake.
Ndugu wanasemaje?
Ndugu wa
marehemu akiwepo dada yake ambaye ndio wa kwanza kuzaliwa, Amida Mohamed Mbegu,
ameiambia Saluti5 kuwa hadi sasa wameadhimia kukubali kazi ya Mungu na
hawatarajii kuufanyia upasuaji mwili wa marehemu ili kujua chanzo cha kifo
chake.
Maisha yake katika siku za hivi
karibuni:
Ndugu wa
marehemu wanasema katika siku za hivi karibu, Aisha alikuwa akiondoka nyumbani
kwao Kigamboni asubuhi na kusema anaelekea kwenye mazoezi ya Twanga Pepeta
kwaajili ya onyesho la miaka 16 ya Luizer Mbutu.
Lakini
kiongozi wa madansa wa Twanga, Danger Boy ameiambia Saluti5 kuwa Aisha Madinda
hajawahi kuonekana kwenye mazoezi ya bendi yao.
Kiongozi wa
Twanga Pepeta, Luzier Mbutu naye amekiri kuwa licha ya Aisha Madinda kumwahidi
mara kadhaa kwa njia ya simu kuwa atashiriki mazoezi, lakini hakuwahi kutokea
hata mara moja.
|
No comments:
Post a Comment