UPDATES ZA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014:-Wilaya ya Ngara huku Kibondo Vitongoji 28 matokeo yakibatilishwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 17, 2014

UPDATES ZA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014:-Wilaya ya Ngara huku Kibondo Vitongoji 28 matokeo yakibatilishwa.

NGARA.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa Desemba 14,2014, wilayani Ngara mkoani Kagera yanaonesha kuwa Chama cha Mapinduzi kinaongoza kikifuatiwa na Chadema huku Chama cha NCCR Mageuzi kikifuatia .

Kaimu Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Ngara Bw Fred Kakuru amesema hadi kufikia jana Desemba 16,2014, katika vijiji vilivyopiga kura 69, Chama cha Mapinduzi kimeshinda vijiji 61, Chadema vijiji vitatu huku NCCR Mageuzi kikipata kijiji kimoja.

Amesema vitongoji 338 vilivyofanya uchaguzi kati ya vitongoji 394 vilivyopo, Chama cha Mapinduzi kimeshinda vitongoiji 294, Chadema vitongoji 43 na NCCR Mageuzi kitongoji kimoja.

Bw Kakuru amesema vijiji vingine vitatu vyenye vitongoji 8 vimefanya uchaguzi leo Desemba 17,2014 na kwamba kijiji cha Mbuba kitafanya uchaguzi Jumapili kutokana na vifaa vilivyotakiwa kupelekwa kwenye kijiji hicho, vilipelekwa sehemu nyingine

KIBONDO.

Msimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Bw Judethadius Mboya amebatilisha matokeo ya uchaguzi kwa wenyeviti wa vitongoji 28 baada ya kubaini kasoro katika vituo hivyo na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

Bw Mboya amezitaja sababu za kubatilisha matokeo hayo kuwa ni kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura tofauti na waliojiandikisha, dosari kwenye karatasi za kupigia kura kwa kubadili majina ya wagombea pamoja na wagombea kulingana kura.

Amesema vituo hivyo 28 vinatarajia kufanya uchanguzi baada ya siku 7 kuanzia sasa ili kutoa fursa kwa wananchi kuchangua upya viongozi wao kulingana na kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi.

Bw Mboya amewataka wakazi wa maeneo ambayo uchaguzi wao umesogezwa mbele kuwa na subira kwa kuwa imefanyika hivyo kwa nia njema.

Habari Na:-Radio kwizera FM-Ngara.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad