DOSARI ZA UCHAGUZI TAMISEMI 2014:- Wakurugenzi hawa wamesimamishwa kazi.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, December 17, 2014

DOSARI ZA UCHAGUZI TAMISEMI 2014:- Wakurugenzi hawa wamesimamishwa kazi..

Siku chache baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Hawa Ghasia kuahidi kumuwajibisha yoyote aliyehusika na kuvuruga uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe 14, leo Desemba 17,2014,Waziri huyo ametangaza majina ya Wakurugenzi watano waliosimamishwa kazi na wengine sita waliopewa onyo kutokana na uchunguzi kuonyesha wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

 Majina ya Wakurugenzi waliotajwa kusimamishwa ni haya; Felix Mabula (Halmashauri ya Hanang), Fortunatus Fwema (Halmashauri ya Mbulu),  Isabella Chilumba (Halmashauri ya Ulanga),  Pendo Malabeja (Halmashauri ya Kwimba) na William Shimwela (Halmashauri ya Sumbawanga).

Ni dhahiri kuwa Wakurugenzi wa kwenye zile Halmashauri zenye dosari wameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo jukumu la msingi la kusimamia uchaguzi ambao ni moja ya majukumu ya Wakurugenzi. Kasoro hizo zilisababisha kurudiwa kwa uchaguzi katika baadhi ya maeneo yao… Wakurugenzi hao wametenda makosa yafuatayo ambayo yanawaondolea sifa ya kuwa wakurugenzi katika halmashauri“– Hawa Ghasia.

Kwanza ni kuchelewa kuandaa vifaa vya kupigia kura, kukosa umakini katika kuandaa vifaa vya kupigia kura na hivyo kuchanganya majina pamoja na vyama, kuchelewa kupeleka vifaa kwenye maeneo ya kupigia kura, uzembe katika kutekeleza majukumu yao na kutoa taarifa za kupotosha kuhusu maandalizi ya uchaguzi.. kwa sababu walituhakikishia kwamba maandalizi yamekamilika huku wakifahamu kwamba suala hilo sio kweli“– Hawa Ghasia.


Waziri Ghasia ametaja Halmashauri ambazo wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda huku Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.

UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad