AISHA MADINDA AZIKWA LEO desemba 19,2014:- Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 19, 2014

AISHA MADINDA AZIKWA LEO desemba 19,2014:- Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Aisha Madinda kuelekea makaburini.

Hatimaye mwili wa aliyekuwa mwimbaji na mnenguaji wa Twanga Pepeta, Aisha Madinda umezikwa leo Desemba 19,2014,jioni kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana Desemba 18,2014 kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.

Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar wamejitokeza na kuhudhuria maziko ya msanii huyo aliyefariki dunia juzi Desemba 17,2014.

Aidha Wakurugenzi  wa bendi hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali Choki, waliwaongoza mamia ya waombolezaji katika msiba huo kumzika Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.

Maziko ya mwili wa marehemu Aisha Madinda yakifanyika katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jioni hii.

Baada ya uchunguzi huo kufanyika na ripoti kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi na familia, mazishi hayo yakafanyika leo Desemba 19,2014,jioni yakihudhuriwa na Asha Baraka na Choki, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Salim Omari Mwinyi.
Akizungumza katika mazishi hayo, Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa African Stars Entertainment inayoimiliki Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, alimuelezea Aisha kuwa ni sawa na mwanaye kutokana na muda mwingi aliotumia akiwa Twanga.

Baraka aliongeza kuwa licha ya kutokuwa na Aisha katika siku za karibuni, bado Twanga Pepeta inatambua na kuthamini mchango wa mkali huyo wa jukwaa na kwamba pengo lake halitasahaulika kirahisi ndani ya bendi hiyo kongwe.

Kwa upande wake Choki alisema daima atakumbuka uwajibikaji, usikivu na upendo wa Aisha akiwa na Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ na kwamba kwake yeye marehemu ni sawa na dada yake, huku akimtaja kama mtumishi mwema.

Alikuwa na Extra Bongo kwa muda mfupi, lakini aina yake ya utumishi utabaki katika kumbukumbu zetu daima. Huu ni mwaka wa taabu kwangu, kwani siku ya arobaini ya marehemu mke wangu, alifariki pia mzee wangu Shem Karenga,” alisikitika Choki.

Choki alienda mbali zaidi kwa kulalama kuwa, siku moja baada ya kumzika Shem Karenga, ndio siku aliyofariki Aisha Madinda, hivyo kuendeleza mfululizo wa majonzi kwake na wadau wa tasnia nzima ya muziki wa dansi nchini.

Kwa upande wake, mtoto wa dada wa marehemu, Sheikh Mohamed Mussa, ambaye aliongoza mazishi upande wa familia, aliwashukuru Watanzania kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha mazishi hayo, huku akiwataka kuuendelea kumuombea.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad