Mheshimiwa
John Mongella Akipokelewa na Katibu Tawala Mkoa Bw. Nassor Mnambila na Kanali
Mstaafu Massawe wakati akiwasili Mkoani Kagera kuanza kazi rasmi.
|
Kwa pamoja
wakitembea Kuelekea Mapokezi Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
|
Akisaini
Kitabu cha Wageni Uwanja wa Ndege wa Bukoba
|
Mkuu Mpya wa
Mkoa Bwana John Mongella Aipokea Nyaraka na Kukabidhiwa Ofisi Rasmi na
Mtangulizi wa Kanali Mstaafu Fabian Massawe.
|
Na;
Sylvester Raphael
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera Bwana John Mongella
aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete
Novemba 5, 2014 kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera amewasili rasmi mkoani hapa na kupokelewa
na kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Kanali Mstaafu Fabian Inyasi Massawe.
Katika hafla fupi leo tarehe
14/11/2014 Kanali Mstaafu Fabiani Massawe alimsomea taarifa ya maendeleo ya mkoa
Mhe. John Mongella na kumkabidhi taarifa hiyo pamoja na taarifa ya utekelezaji
wa bajeti ya serikali katika mkoa wa Kagera mwaka wa fedha 2014/15, na taarifa
ya malengo ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2014/15.
Kanali Massawe pamoja na
kusoma na kukabidhi taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Kagera hakusita kuzitaja
changamoto zinazoukabili mkoa kwa sasa ambazo ni Wahamiaji haramu hasa katika wilaya za Ngara, Kyerwa,
Karagwe na Missenyi. Magendo ya mazao na hasa kahawa, nafaka, mazao ya misitu,
bidhaa mbalimbali hufanyika kwenda nchi jirani.
Kilimo chetu
kinakabiliwa na uzalishaji mdogo (tija); matumizi duni ya pembejeo na zana za
kilimo; uhaba wa maafisa ugani na magonjwa hatari ya mimeaUfugaji nao bado ni
wa kiasili wa ng’ombe aina ya ankole ambao uzalishaji wake wa nyama na maziwa ni
duni:
Upungufu wa miundombinu ya mifugo kama majosho; magonjwa ya mifugo. Wavuvi
wengi kutumia zana za asili kuvulia samaki. Michango ya halmashauri
katika bajeti zake ni kati ya 2% hadi
4% ya bajeti nzima ya Halmashauri hizo.
Kwa hiyo hali ya utegemezi ni kubwa sana na hii inazipunguzia uwezo wa
kuchangia katika maendeleo na utoaji wa huduma za kuridhisha.
Akikiri kupokea ofisi na
kuanza kuchapa kazi kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera Mkuu wa mkoa
Mheshimiwa John Mongella alihaidi
kuendeleza jitihada alizokuwa akizifanya Kanali Massawe katika kuwaletea
wananchi maendeleo kwa kushirikiana na
watendaji walioko chini yake na wadau mbalimbali wa mkoa.
Pili, Mhe. Mongella alitoa
angalizo kwa watendaji wa serikali kuhakikisha wanawahudumia wananchi katika
ofisi zao bila kutumia milolongo mirefu ya sheria na taratibu. “Mwananchi hajui
mambo ya standing order anachojali ni kupata huduma kwa wakati bila
kucheleshwa, kwahiyo punguzeni milolongo mirefu ya utendaji wa kazi katika
kutoa huduma.” Alisistiza Mhe. Mongella.
Tatu, Mkuu wa Mkoa Mongella
alisistiza kuwa hapendi kufanya kazi kwa maneno mengi bali kwa vitendo na kuona
, “Kama ni vyumba vya maabara nataka kuonyeshwa vyumba au kama ni zahanati
nataka kuonyeshwa zahanati na siyo maneno maneno tu.” Aliongeza Mkuu wa Mkoa Mongella.
Mwisho Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe. John Mongella alikemea na kutoa angalizo kuacha kutumia siasa au
kuendekeza siasa katika maendeleo ya wananchi, alisema waache wanansiasa
wafanye siasa zao lakini si katika kuwaletea wananchi maendeleo ambalo ndilo
jukumu kuu la viongozi na watendaji wa serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
John Mongella kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha na anakuwa Mkuu wa Mkoa
wa Kagera wa tangu uhuru mwaka 1961.
No comments:
Post a Comment