 |
Moshi ukiwa
umetanda angani Wakati Moto mkubwa
uliozuka leo November 14,2014, mchana katika jengo la biashara Machinga Complex Ilala jijini Dar
es salaam, umedhibitiwa baada ya kutekeza mali katika baadhi ya maduka.
Mwenyekiti
wa bodi ya usimamizi wa jengo la Machinga Complex, Godwin Mmbaya amesema moto
huo umedhibitiwa na hali ni shwari.
|
 |
“Tunashukuru
Mungu moto umedhibitiwa kabla haujasambaa zaidi, kikosi cha zimamoto kiliwahi
mapema na kilisaidia kufanikisha kuzima moto. Hakuna mtu alieyeumia zaidi ya
kuteketea kwa mali kwenye maduka ambayo moto ulitokea, bado hatuna tathimini ya
mali zilizoteketea, chanzo cha moto ni fundi alikuwa anakata kitu na mashine
sasa vile cheche zikadondokea kwenye kitu, moto ukatokea na kuchanganya, sisi
kwanza tunawapa pole wale wote waliopotelewa na mali zao kwa moto,” alisema
Godwin.
Katika hatua
nyingine Godwin alisema material yaliyotumika kujengea jengo hilo ni material
ambayo hayawezi ungua na moto hali iliyosaidia moto huo kutosambaa mbali zaidi
|
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa
kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu
>>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa
WhatsApp
Make Money at :
http://bit.ly/adflywin
No comments:
Post a Comment