Bwana Rogers
akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi.
Juliana
alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi
alipokuwa akielekea soko la Sido kwenye shughuli zake za biashara na kutoa
taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa na baadaye kituo kikuu kati na kufunguliwa
jalada la wizi wa mtoto namba MB/RB/9384/2014 ambapo juhudi za kumtafuta
zilifanikiwa baada ya taarifa kutolewa Kituo cha Radio cha Bomba FM Mbeya ndipo
alipojisalimisha mwenyewe akiwa na mtoto Zalida Rogers(2).
Hata hivyo
katika hali ya mshangao Biton alifika katika kituo cha Polisi Kati akiwa na
Cheti cha kuzaliwa na kadi ya kliniki ambapo kinaonesha mtoto Zalida kuzaliwa
kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa na kuonesha kuzaliwa 18/08/2012 wazazi wakiwa
ni Juliana Josia na Biton Mwashilindi.
Biton alidai
mbele ya Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi kuwa Juliana ni mpenzi wake kwa
muda wa miaka nane na kwamba walikuwa wakikutana katika nyumba ya kulala wageni
kila alipomhitaji na walikuwa wakipanga katika nyumba hiyo kwa siku saba kila
wanapokutana hali ilyofanya watu wanaosikiliza tukio hilo kituo cha Polisi
kushikwa na butwaa akiwemo mume halali Rogers Halinga na mke wa Biton ambaye
alimtunza mtoto kwa siku nne.
Akijieleza
kwa kujiamini Biton alidai kuwa hata mtaji wa biashara alimpatia yeye na hata
wazazi wake Biton walioko Itaka Mbozi walimtambua mtoto Zalida na kwamba jina
la mtoto alipewa na ndugu zake na hata aliowahi kuugua alikwenda Itaka Mbozi na
kukaa kwa wazazi wa Biton kwa zaidi ya juma moja.
Kwa upande
wa Rogers yeye alisema mtoto Zalida ni wa kwake na kwamba aliondoka kwao
akiwana na ujauzito wa miezi mitano na kwamba yeye alijua kukorofishana kwao
kulitokana na hali ya ujauzito na alikaa kwamba mkewe Juliana alikaa kwao
kwa miezi sita na alipojifungua alirejea kwake na aliohitaji kupata maendeleo
ya mtoto mkewe alidai kuwa kadi ya kliniki imepotea.
Kikao hicho
kilichokuwa na mvutano mkubwa kiliahirishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya
kwa kumshikilia Biton kwa kosa la kutorosha mtoto na kesi ya ugoni na kuwa
atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika huku Rogers akikabidhiwa
mkewe na mtoto kwa minjili ya kwenda kuyajenga huko nyumbani kwao Kijiji cha
Ishungu Kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali.
Baba mzazi
wa Rogers Mzee Jason Halinga alisema alishangazwa na kitendo kilichofanwya na
mwanamke huyo ambapo alidai kuwa mwanae alioa kihalali na kufuata mila zote na
kulipa mahari lakini alishangazwa na kitendo cha wazazi wa Juliana kushindwa
kuonesha ushirikiano hali inayoashiria kujua kile kilichokuwa kinafanywa na
mtoto wao.
Biton
alifika kituo cha Polisi akiwa na mkewe wa ndoa ambapo naye hakufahamu kuwa
mumewe anaishi na mke mwingine nje ya ndoa na kwamba mtoto Zalida alipoletwa
kwake hakuambiwa chochote kile na kwamba ameishi kwenye mateso ya ndoa kwa muda
wa miaka nane huku akifanyiwa vitendo vya kikatili na mumewe ikwa pamoja na
kuambulia kipigo mara kwa mara.
Baadhi ya
ndugu wa Rogers walioneshwa kukerwa na baadhi ya Askari wa ngazi juu
katika Dawati la Jinsia Kituoni hapo ambao walonesha kutojali suala hili huku
wakitioa maneno ya kejeli hali inayotia dosari utendaji kazi wa Dawati hilo na
kwamba lipo kibiashara zaidi na si huduma kama ilivyo sera ya Jeshi la
Polisi.
Hata hivyo
hawakusita kuwapongeza Askari wa Kiume walionesha juhudi hata kufanikwa
kupatikana kwa mtoto Zalida na Biton pamoja na rafiki yake.
Katika
sakata hili kama si juhudi za Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi
kuingila kati basi mtoto Zalida asingeweza kupatikana kama baadhi ya watoto
waliotoweka maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambao hawajapatikana mpaka sasa
ambapo wananchi wamelalamikia Kituo Kikuu cha Kati kwa kutochukua hatua za haraka
za kukomesha vitendo vya ukatili wa Kijinsia na baadhi kuamua kumalizana
wenyewe mitaani vikiwemo vitendo vya ubakaji ambavyo vimeshamiri mkoani Mbeya.
Hatima ya
ndoa ya Rogers na Juliana itajulikana baada ya mazungumzo yatayofanyika kwa
Mzee Jason Halinga nyumbani kwake Ishungu Kata ya Ruiwa hivi karibuni kikao
kitakutaniha pande mbili za wazai ili kufikia muafaka katika sakata la aina
yake na kwamba hata kubainika kwa sula hili ni kutokana na Juliana kufumwa na
mwanaume mwingine katika chumba ambacho Biton alikuwa awe na Juliana ndipo
alipoamua kulipiza kisasi kwa kutorosha mtoto.
Na Mbeya
yetu
|
No comments:
Post a Comment