![]() |
Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru wafanyabiashara watatu, wakiwemo mume na
mke, waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 13 na miezi sita jela kwa sababu
ya wizi wa Sh bilioni 1.1 katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya (EPA) ya Benki Kuu
ya Tanzania (BoT).
Walioachiwa
huru ni mume Manase Makale na mkewe Edda Makale, na mfanyabiashara mwingine
Bahati Mahenge.
Washitakiwa
hao waliachiwa mwisho wa wiki iliyopita baada ya Jaji Augustine Shangwa
kukubali rufaa iliyowasilishwa na wafanyabiashara hao kupinga hukumu
iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka jana.
Akisoma
hukumu hiyo, Jaji Shangwa alisema anawaachia huru wafanyabiashara hao kwa kuwa
upande wa Jamhuri ulishindwa kabisa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Aliamuru
wafanyabiashara hao waachiwe huru mara moja na kutengua amri ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu iliyowataka warejeshe fedha hizo mara baada ya kutumikia
kifungo.
Katika
rufaa, wafanyabiashara walikuwa wakipinga hukumu iliyotolewa na jopo la
mahakimu Sekela Mushi, Sam Rumanyika na Lameck Mlacha, wakidai kuwa kulikuwepo
na upungufu mkubwa wa kisheria na kihoja katika kuwatia hatiani.
Katika
hukumu iliyotolewa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mahenge alitakiwa kutumikia
kifungo cha miaka saba jela, Makale kifungo cha miaka mitano jela na mkewe Edda
kifungo cha mwaka mmoja na nusu.
Aidha,
mahakama iliamuru baada ya kutumikia adhabu hiyo, Mahenge na Makale warejeshe
kiasi cha Sh bilioni 1.18 walichodaiwa kukiiba katika akaunti ya EPA.
Washitakiwa
walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kula njama ya kutenda kosa, kughushi
nyaraka mbalimbali na kuziwasilisha sehemu husika na kuiba fedha hizo.
Katika kesi
hiyo, wafanyabiashara hao walikuwa wameshitakiwa na wenzao Davis Kamungu na
Godfrey Mushi ambao waliachiwa huru katika Mahakama ya Kisutu kwa kuwa upande
wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao bila kuacha shaka.
Chanzo: Habari Leo.
Karibu kwenye familia
ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku
baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA
HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
Copy n Win at: http://bit.ly/copyandwin |
Karibu kwenye familia
ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku
baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA
HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
Copy n Win at: http://bit.ly/copyandwin
Copy n Win at: http://bit.ly/copyandwin
No comments:
Post a Comment