LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Tazama Penati ya Hazard ikiipa Chelsea ushindi wa 2-1 leo November 1, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, November 01, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Tazama Penati ya Hazard ikiipa Chelsea ushindi wa 2-1 leo November 1, 2014.

Vinara wa Ligi Kuu Uingereza, Chelsea, Leo November 01,2014,wamerudi tena kwenye wimbi lao la ushindi kwa kuifunga QPR Bao 2-1 huku bao la ushindi likifungwa na Eden Hazard kwa Penati ya Dakika ya 75 kwenye Mechi iliyochezwa Stamford Bridge.

 Chelsea walipata Bao la kwanza Fakika ya 32 Mfungaji akiwa Oscar na QPR kusawazisha Dakika ya 62 kwa Bao la Charlie Austin.

Lakini walishinda Mechi hii baada ya kupewa Penati kufuatia Hazard kuchezewa Faulo na Eduardo Vargas.

Huko Emirates, Arsenal wamechupa hai Nafasi ya 4 kwenye Ligi kwa kuichapa Burnley Bao 3-0 kwa Bao zote za Kipindi cha Pili.

Alexis Sancheza aliifungia Arsenal Bao 2, Dakika za 70 na 90, na Callum Chambers kupiga moja Dakika ya 72.

Jumapili November 02,2014.

1630 Man City v Man United

1900 Aston Villa v Tottenham

Jumatatu Novemba 03,2014.

2300 Crystal Palace v Sunderland
 


MSIMAMO EPL 2014/2015.

NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
10
16
26
2
Southampton
10
16
22
3
Man City
9
9
17
4
Arsenal
10
7
17
5
West Ham
10
5
17
6
Swansea
10
3
15
7
Liverpool
10
0
14
8
Man United
9
3
13
9
West Brom
10
0
13
10
Everton
10
2
13
11
Newcastle
10
-4
13
12
Stoke
10
-2
12
13
Hull
10
-1
11
14
Tottenham
9
-2
11
15
Aston Villa
9
-10
10
16
Crystal Palace
9
-3
9
17
Leicester
10
-5
9
18
Sunderland
9
-9
8
19
QPR
10
-11
7
20
Burnley
10
-14
4

Wakicheza Uwanjani kwao Saint James Park, Nao Newcastle wameifunga Liverpool Bao 1-0 katika Mechi ya Ligi Kuu.

Huu sasa ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Meneja wa Newcastle Alan Pardew na kukata ngebe za wale Mashabiki waliotaka atimuliwa kwa kuanza Msimu vibaya.

Bao la ushindi la Newcastle lilifungwa Dakika ya 73 na Ayoze Pérez Gutiérrez kutokana na Krosi ya Paul Dummett ambayo Liverpool walishindwa kuiokoa.

Hii ni Mechi ya 8 kwa Straika wa Liverpool Mario Balotelli kucheza na kutofunga Bao kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad