KATIBA MPYA TANZANIA:- Taswira ya Picha 4 za Vurugu zilivyo vunja Mdahalo na Jaji Warioba kunusurika Kipigo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 02, 2014

KATIBA MPYA TANZANIA:- Taswira ya Picha 4 za Vurugu zilivyo vunja Mdahalo na Jaji Warioba kunusurika Kipigo.

Pichani ni Mzee Warioba akitolewa nje baada ya vurugu zilizojitokeza kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba,uliofanyika leo November 2, 2014, Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.


Vurugu zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea leo November 02,2014,katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.

Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.

Mdahalo huo uliokuwa unahusu Elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kushirikisha waliokuwa makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Joseph warioba.

 Jaji warioba ndiye aliyekuwa wa kwanza kuichambua Katiba inayopendekezwa, na kuelezea mapungufu kadhaa ikiwa ni pamoja na masuala ambayo Bunge La Katiba limeyaacha kutoka katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume hiyo.

Katika maelezo yake, Jaji Warioba ameeleza kusikitishwa kwake na kuachwa kwa mambo ya muhimu ikiwa ni pamoja na miiko ya uongozi pamoja na Tunu za Taifa, lakini amepongeza baadhi ya mambo kuboreshwa ikiwa ni pamoja na Haki za Binadamu.

Wakati akielezea umuhimu wa kuweka miiko ya uongozi kwenye Katiba, ndipo baadhi ya vijana wakatoa mabango yenye ujumbe wa kupinga hotuba ya Warioba na kuunga mkono katiba inayopendekezwa. 

Bango mojawapo lilisomeka “TUMEIPOKEA, TUNAIKUBALI NA TUNAIUNGA MKONO KATIBA PENDEKEZWA

Baada ya hapo kilichofuata ni vurugu zilizoambatana na mapigano miongoni mwao kati ya wanaounga mkono katiba na wanaopinga.
 

Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV ulisimamishwa kwa muda.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad