LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Yaliyojiri Man United na Man City leo November 2, 2014, hii ni mara ya ngapi kwa City kuifanyia United? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, November 02, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Yaliyojiri Man United na Man City leo November 2, 2014, hii ni mara ya ngapi kwa City kuifanyia United?

Goli  la Dakika ya 63 la Sergio Aguero limewapa Manchester City ushindi wa Nyumbani , Etihad kwenye Dabi ya Jiji la Manchester walipoifunga Manchester United kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza leo November 2, 2014.

 Man United walibakia Mtu 10 kuanzia Dakika ya 39 wakati Sentahafu wao Chris Smalling alipotolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kupokea Kadi za Njano mbili.
Mbali ya pigo hilo, Man United walipata pigo jingine wakati Sentahafu wao mwingine Marcos Rojo kutolewa nje alipoumia Bega kwenye Dakika ya 56 na kuiacha Man United ina Difensi ya kuungaunga ya Antonio Valencia, Michael Carrick, Chipukizi wa Miaka 19 Paddy McNair na Luke Shaw.

Hii ilikuwa Mechi ya kwanza ya Ligi kwa Carrick tangu Msimu uanze baada ya kuumia enka.

Licha ya mapigo hayo ya Uwanjani, Man United pungufu ilicheza vizuri mwishoni na wangeweza kuambulia hata Sare.

Ushindi huu umeiweka Man City Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Southampton walio Nafasi ya 2 na Pointi 6 nyuma ya Vinara Chelsea.Man United wamebaki Nafasi ya 9.

Sergio Aguero akishangilia bao lake alilofunga dakika ya 63 dhidi ya Manchester United. 

Huu ni ushindi wa nne mfululizo ambao City inaupata mbele ya United huku Sergio Aguerro akiendelea kuwaumiza mashetani wekundu akiwa tayari amefunga magoli matano kwenye michezo sita dhidi ya United.
MSIMAMO EPL 2014/2015.

NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
10
16
26
2
Southampton
10
16
22
3
Man City
10
10
20
4
Arsenal
10
7
17
5
West Ham
10
5
17
6
Swansea
10
3
15
7
Liverpool
10
0
14
8
Everton
10
2
13
9
Man United
10
2
13
10
West Brom
10
0
13
11
Newcastle
10
-4
13
12
Stoke
10
-2
12
13
Hull
10
-1
11
14
Tottenham
9
-2
11
15
Aston Villa
9
-10
10
16
Crystal Palace
9
-3
9
17
Leicester
10
-5
9
18
Sunderland
9
-9
8
19
QPR
10
-11
7
20
Burnley
10
-14
4
 
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad