Mwenyekiti
wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Paul Makonda,
aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu.
Lakini alipoulizwa na BBC
kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema kwamba
alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati wa
vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa kauli za
kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya iliyokuwa
ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana
maelezo ya kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
Tanzania ipo
katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na kupitishwa na
bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa kupigiwa kura na wananchi
mwezi Aprili, 2015.
Wachambuzi
wa maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na kuvumiliana
hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta ghasia ambazo zinaweza
kuepukika.
|
No comments:
Post a Comment