PICHA:-Ndani ya Birthday Party ya Diamond Platinumz na zawadi ya BMW aliyopewa October 02,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, October 04, 2014

PICHA:-Ndani ya Birthday Party ya Diamond Platinumz na zawadi ya BMW aliyopewa October 02,2014.


Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz au Nasibu Abdul Juma alizaliwa October 2 ,1989 ambapo akiwa darasa la tano ndio akaanza kuonyesha kwamba anaupenda muziki ambao miaka kadhaa baadae ndio umekuja kuikomboa familia yake na yeye mwenyewe kuweza kuishi maisha mazuri.

 Kwenye hii party ambayo ilifanyika Golden Jubilee Towers Dar es salaam Kilimanjaro hall, October 02,2014,usiku, ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Tanzania wakiwemo Waigizaji, Watangazaji wa Radio na TV, Wasanii wa bongofleva na wengine.

Diamond Platinumz jana usiku alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 25.

Sherehe hiyo ilifana ambapo mama yake mzani na mpenzi wake Wema Sepetu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria waliinogesha sherehe hiyo iliyomalizika majira ya saa kumi alfajiri.



Meneja wa Diamond, Babu Tale amesema party hiyo iligharimu shilingi milioni 28 na kuwataja waliohusika kuigharamia.
“Event tumefanya wenyewe lakini mwisho wa siku Diamond yupo karibu na watu wengi na makampuni mengi”. Tale ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “Coca cola kama Coca Cola ndio walichukua nafasi kubwa kuifanya ile event sababu wao ni balozi wao….ilikuwa gharama inagharimu milioni 28 kwa sisi wenyewe watoto wa paka tusingeweza kuitoa kirahisi hiyo hela.”







Pamoja na zawadi nyingine, Menejiment ya Diamond ilimpa zawadi ya gari jipya aina ya BMW X6.

Zawadi kubwa aliyopata Diamond kwenye birthday yake ni gari aina ya BMW X6, ambayo alipewa na uongozi wake unaoundwa na Babu Tale, Said Fela na Salam. Tale ameelezea jinsi walivyoweza kupata pesa za kununua gari hiyo.

“Sasa hivi Diamond anafanya vizuri na tulikuwa tunamwambia Diamond kwamba kuna contract tukisaini tutakupa zawadi, as in kwamba management haitachukua percent ya hiyo contract hiyo pesa itaenda kwenye kukuchukulia wewe zawadi, akasema nyie bana mlivyokuwa watata sijui kama mtakubali.”
Aliendelea,

“Tulivyotoka South Africa tukawa kuna contract tume confirm kusaini, tulivyosaini ile contract ile pesa ambayo ilitakiwa pasenti yote ije kwetu sisi mimi, Fela na Salam yote tukasema tumchukulie zawadi….ni shilingi ya kitanzania milioni 90”.
  -bongo5
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad