|
Hapo kesho
Jumamosi October 18,2014, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utarindima kwa
Dabi ya Kariakoo wakati Vigogo wa Soka Nchini Tanzania na Watani wa Jadi, Yanga
SC na Simba SC, watakapovaana katika pambano lao la kwanza la Ligi Kuu Vodacom
kwa Msimu wa 2014/15.
Watani hao
wanatinga kwenye kimbembe hiki kinachongojewa Nchi nzima hasa kwa vile Msimu
huu kila Timu ina Benchi la Ufundi jipya kwa Yanga kuwa na Kocha wa zamani wa
Timu ya Taifa ya Tanzania kutoka Brazil Marcio Maximo, na Simba kuongozwa na
Kocha wao wa zamani Mzambia Patrick Phiri.
|
|
Vile vile
mvuto zaidi ni ule wa kuona Wabrazil wa Yanga SC, Kiungo Andrey Ferreira Coutinho
na Geilson Santos ' Jaja' wakivaana na Simba SC iliyomteka Straika wa Yanga,
Mganda Emmanuel Okwi.
Hii itakuwa
Mechi ya 4 ya Ligi kwa kila Timu lakini Yanga SC wanaingia wakiwa Nafasi ya 3
wakiwa na Pointi 6 wakati Simba SC wako Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 3.
Msimu huu,
Yanga SC walianza kwa kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda
Mechi mbili mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa Bao 2-1 kila moja.
Simba SC wao
hawajafungwa lakini hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa
kutoka Sare na 2-2 na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na
Polisi Morogoro.
Refa wa
mtanange huu wa Jumamosi ni Israel Nkongo ambae atasaidiwa na Ferdinand Chacha
na John Kanyenye wakati Hashim Abdallah atakuwa Refa wa Akiba na Kamishna ni
Salum Kikwamba.
Msimu uliopita,
Refa Israel Nkongo ndie aliesimamia Mechi ya Mahasimu hawa ambapo Yanga
SC waliongoza 3-0 hadi Mapumziko na Simba SC kuweza kurudisha na kupata Sare ya 3-3.
|
|
Nao Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Azam FC watakuwa na
kibarua kigumu mbele ya Mbeya City ambao hawajafungwa hata goli moja msimu huu
wakati timu hizo zitakapovaana kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya keshokutwa.
Azam FC ambao mpaka sasa wamecheza mechi 37 za Ligi bila kufungwa ikiwa Nane za
msimu wa 2012/13, 26 za msimu uliopita 2013/2014 na tatu za msimu huu 2014/2015,
watashuka kwenye uwanja huo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa na kumbukumbu
ya kuibuka na ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya ‘wababe’ hao, ushindi ambao uliwapa
Ubingwa wa VPL Machi 23,mwaka jana wakiwa mechi moja mkononi.
RATIBA
LIGI KUU VPL 2014/2015.
Jumamosi
Oktoba 18,2014.
Polisi Moro
v Mtibwa Sugar
Ndanda FC v
Ruvu Shooting
Kagera Sugar
v Stand United
Coastal
Union v Mgambo JKT
Mbeya City v
Azam FC
Yanga SC v
Simba SC
Jumapili
Oktoba 19,2014.
Prisons v
JKT Ruvu
|
MSIMAMO LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2014/2015.
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Mtibwa Sugar
|
3
|
3
|
0
|
0
|
6
|
1
|
5
|
9
|
2
|
Azam FC
|
3
|
2
|
1
|
0
|
5
|
1
|
4
|
7
|
3
|
Yanga
|
3
|
2
|
0
|
1
|
4
|
4
|
0
|
6
|
4
|
Mbeya City
|
3
|
1
|
2
|
0
|
1
|
0
|
1
|
5
|
5
|
Tanzania Prisons
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2
|
1
|
4
|
6
|
Kagera Sugar
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2
|
1
|
4
|
7
|
Coastal Union
|
3
|
1
|
1
|
1
|
4
|
4
|
0
|
4
|
8
|
Stand United
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
5
|
-2
|
4
|
9
|
Ndanda FC
|
3
|
1
|
0
|
2
|
6
|
6
|
0
|
3
|
10
|
Simba
|
3
|
0
|
3
|
0
|
4
|
4
|
0
|
3
|
11
|
Mgambo JKT
|
3
|
1
|
0
|
2
|
1
|
2
|
-1
|
3
|
12
|
Polisi Moro
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
5
|
-2
|
2
|
13
|
JKT Ruvu
|
3
|
0
|
1
|
2
|
1
|
4
|
-3
|
1
|
14
|
Ruvu Shooting
|
3
|
0
|
1
|
2
|
0
|
4
|
-4
|
1 |
Karibu
kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana
/Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment