KUMUENZI MWALIMU JK NYERERE:- Wanamichezo Ngara waadhimisha kwa Mchezo wa Drafti ,Mshindi wa mwisho kaondoka na Mchicha,Vitunguu na Nyanya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 15, 2014

KUMUENZI MWALIMU JK NYERERE:- Wanamichezo Ngara waadhimisha kwa Mchezo wa Drafti ,Mshindi wa mwisho kaondoka na Mchicha,Vitunguu na Nyanya.

Washindi wane bora wa shindano la mchezo wa Drafti wenye lengo la kumuenzi Hayati Baba wa Taifa ,Mwalimu Nyerere October 14,2014,Lilianza October 11,2014 na fainali yake kufanyika October 14,2014 katika eneo la Fred Shop mjini Ngara.

 Watanzania hapo Jana October 14,2014,wameadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 kwa michezo mbalimbali , ikiwa ni tangu kifo cha baba wa taifa  letu,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye aliaga dunia October 14,1999.

Siku hiyo ilikua ni siku ya mapumziko kwa watanzania ,wakati huu ambapo wananchi wametakiwa kuendelea kuyaenzi  yale mazuri aliyowaachia hayati baba wa taifa  ambaye wakati wa uhai wake katika michezo alipendelea sana kucheza mchezo wa bao.
Katika kusisitiza kuuenzi mchezo huo,Wilayani Ngara mkoani Kagera,Jumla ya wachezaji 16 wamekutana katika pambano la mchezo wa drafti na kupatikana washindi 4 bora walioondoka na zawadi.

Msimamizi wa Mchezo huo Stanslausi Basheka amewataja washindi kuwa ni Juma aliyeshinda kwa pointi 29 na kuondoka na Kondoo,wa pili ni Selemani kwa pointi 28 aliondoka na Kuku Jogoo na watatu ni Omera aliyeondoka na Kuku Jike baada ya kushinda kwa pointi 26.

Mshindi wa nne ni Simon alishinda kwa pointi 25 na kuondoka na Kuku Jike.
Msimamizi wa Mchezo huo wa Drafti,Stanslausi Basheka kulia akiweka mambo sawa kabla ya kutangaza Washindi.
Aidha zawadi zote hizo zilizoambatana na unywaji wa vinyaji kwa washiriki zimegharimu jumla ya shilingi Laki 3.

Mchezo huo wa Drafti wenye lengo la kumuenzi Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere umefadhiriwa na Wafanyabiashara Fred Michael Gahanga na Iman Sempiga na kutoa wito kwa washiriki hao kujiunga pamoja ili kuwa na klabu itakayoleta ushindi na kuhamasisha mchezo wa Drafti wilayani Ngara.
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad