PICHA/SOMA:-Taswita ya Kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Bukombe kilivyovamiwa na Majambazi Usiku wa September 06,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 07, 2014

PICHA/SOMA:-Taswita ya Kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Bukombe kilivyovamiwa na Majambazi Usiku wa September 06,2014.


Wananchi wakiwa wamesimama pembeni ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Bukombe kilichopo Ushirombo, mkoani Geita baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi  usiku wa kuamkia Septemba 06,2014 na kuua askari wawili na kuiba silaha za moto.


 Kituo cha Polisi cha Bukombe mkoani Geita kikiwa kimezungushiwa uzio unaozuia mtu yeyote kuingia ndani ya eneo hilo baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Usiku wa saa 9,Septemba 06,2014,ambapo inadaiwa wahalifu hao ambao idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya kumi, walivamia kituo wakiwa na silaha za kivita.


Kwa mwaka huu 2014, tukio kama hilo la kuvamiwa kwa Kituo cha Polisi na kuuawa kwa askari na majambazi kuchukua silaha ni la pili ambapo la kwanza lilitokea Juni, mwaka huu katika Kituo kidogo cha Polisi cha Mkamba, wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambako majambazi walimuua askari mmoja na kuwajeruhi wengine watatu na kupora silaha tano zenye risasi ambazo ni SMG mbili na Shot gun tatu.

Hata hivyo, wahalifu waliohusika na tukio hilo walikamatwa na kesi yao bado inaendelea. 

Ingawa taarifa ya Jeshi la Polisi nchini haikueleza idadi ya silaha zilizoibwa, taarifa za ndani zinasema majambazi hao wameiba bunduki kumi, risasi na mabomu ya mkono, kisha kutokomea.

Hilo ni tukio la pili kwa askari wa kituo hicho kuuawa na majambazi ambapo Juni 28, 2009 kundi la majambazi saba wenye silaha za moto aina ya SMG, yaliteka magari manne ya mizigo katika pori linalounganisha maeneo ya Runzewe, Matabi na Buselesele lililopo Bukombe na kumuua askari Pascal wa Kituo hicho cha Polisi Bukombe.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP. Ernest Mangu amesema zawadi ya shilingi millioni 10 itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao na silaha zilizoibiwa.
 
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad