SOMA HII KUTOKA KAGERA:-Ni Jeshi la Polisi kunasa Watu wanne kwa tuhuma za kuua kishirikina kisha kupata Ujira. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 13, 2014

SOMA HII KUTOKA KAGERA:-Ni Jeshi la Polisi kunasa Watu wanne kwa tuhuma za kuua kishirikina kisha kupata Ujira.


Picha Na Maktaba Yetu...Jeshi la Polisi mkoani Kagera, inashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukodiwa kufanya mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.

 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alidai kwamba uchunguzi wa jeshi hilo, umebaini watuhumiwa hao wamekuwa wakikodishwa na watu mbalimbali kufanya mauaji na kupewa ujira wa kazi hiyo.

Alitaja watuhumiwa hao kuwa ni Maxmilian PhilMathias (25), Mkombozi Michael (40), Tumaini Basisili (27) na Buhu Mtunzi (34), wote wakazi wa wilayani Biharamulo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe.

Hata hivyo Kamanda Mwaibambe amesema makazi hayo si ya kudumu kwani wamekuwa wakihamahama mara kwa mara.

Alisema watu hao walikamatwa Septemba 10 mwaka huu, saa sita usiku huko Biharamulo kutokana na msako uliofanywa na jeshi la polisi baada ya kupata taarifa za kiintelijensia.

Imeelezwa kuwa wauaji hao walikuwa wakifanya mauaji hayo katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita na Simiyu pia walihusika na tukio la bibi kizee moja aliyeuawa Aprili mwaka huu wilayani Biharamulo.

Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad