SIASA TANZANIA:- Chama cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT’ Chapokea Wanachama Wapya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 30, 2014

SIASA TANZANIA:- Chama cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT’ Chapokea Wanachama Wapya.

Mwanachama wa zamani wa Chadema, Bi.Batuli Abdallah  akijieleza mbele ya wanahabari (hawako pichani)leo Septemba 30,2014.

Yassin Bahama aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chadema akizungumza.
Mohamed Ngulangwa aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) akivaa fulana ya chama hicho.
Mwenyekiti  wa ACT,  Hamis Chambuso akiwa ameshika kadi za Chadema zilizorudishwa na wanachama hao wapya.
Wajumbe na wanahabari wakiwa mkutanoni.

Chama cha siasa hapa nchini Tanzania cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT, leo Septemba 30,2014,kimewapokea wanachama wapya ambao wamehama toka vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Waliopokelewa ni  Yassin Bahama aliyekuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa matofalini,  Ujiji Kigoma, Batuli Abdallah aliyekuwa Katibu  Mwenezi Bavicha katika Jimbo la Kawe, Ofisa na mwasisi  wa chama cha Chauwa,  Sylvester Kasonga pamoja na Engineer Mohammed Ngulangwa toka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza  mbele ya GPL, eneo la Msasani Club, jijini Dar, Mwenyekiti  wa Mkoa wa ACT, Hamis Chambuso amewakaribisha na kuwapongeza  wanachama hao wapya kwa hatua waliyoichukua.

(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad