|
Mwanamke wa Mexicana, Leandra Becerra mwenye umri wa miaka 127 anaetajwa
kuwa mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ameeleza siri ya kuishi miaka mingi
zaidi.
Kwa mujibu wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 45, bibi huyo alimueleza
kuwa siri ya ‘yeye’ kuishi miaka mingi ni kula vizuri, kulala kwa muda
mrefu na kuishi bila kuolewa.
Bi Leandra ambaye alizaliwa August 31, 1887 alikuwa mpiganaji wakati wa
mapinduzi ya Mexico mwaka 1910-1919 na alikuwa kiongozi wa kundi la ‘Adelitas’
ambalo lilikuwa linaundwa na wanawake wanaoenda vitani na waume zao.
Bibi huyo ambaye ana wajukuu wengi huku mjukuu wake mkubwa akiwa na umri
wa miaka 73, tayari ameshawazika watoto wake watano.
Mjukuu wake aliiambia gazeti la El Hozizonte la Mexico kuwa bibi huyo
hivi sasa anatatizo la kubwa la kusikia.
Ameeleza kuwa bibi huyo mara nyingine hulala mfululizo kwa muda wa siku
tatu huku akipewa chakula pale anaposhituka. Lakini akiamka hupenda kula mlo
kamili kwa uhakika, kuimba, kutaniana na kusimulia hadithi mbalimbali
zinazohusu maisha na mapambano ya mapinduzi ya Mexico.
|
Tofauti na
wazee wengi, Bi Leandra yeye hana tatizo la sukari hivyo anakula vitu vya
sukari na chocolate kadri awezavyo.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
No comments:
Post a Comment