LA LIGA 2014/2015:- Ronaldo apiga bao 4 wakati Real Madrid ikishinda 5-1 mchezo wa Ligi Septemba 23,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 24, 2014

LA LIGA 2014/2015:- Ronaldo apiga bao 4 wakati Real Madrid ikishinda 5-1 mchezo wa Ligi Septemba 23,2014.

Mabingwa wa Ulaya 2013/2014, Real Madrid, Jumanne Septemba 23,2014,Usiku walikuwa kwao Santiago Bernabeu na kucheza Mechi ya La Liga na Elche CF na kuitwanga Bao 5-1 huku Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo akipiga Bao 4.

 Hii ni Mechi ya Pili mfululizo kwa Real Madrid kushinda kwa kishindo baada ya Jumamosi kuichakaza Deportivo La Coruna Bao 8-2.

Elche CF walitangulia kufunga kwa Penati ya Dakika ya 15 aliyopiga Edu Albacar na Real Madrid kujibu mapigo kwa Bao za Gareth Bale, Dakika ya 20, na za Cristiano Ronaldo, Dakika ya 28 kwa Penati na Dakika ya 32.

Kipindi cha Pili, Ronaldo alipiga Bao lake la 3 la Mechi na la 4 kwa Real baada ya yeye mwenyewe kuangushwa ndani ya Boksi na Pašalić na kuamriwa Penati aliyofunga.

Hiyo ni Hetitriki ya 25 kwa Klabu yake Real Madrid na kwenye La Liga, Ronaldo amefikisha Hetitriki 21 na amebakisha 1 tu kufikia Rekodi inayoshikiliwa kwa pamoja na Alfredo Di Stefano na Straika wa Athletic Club, Telmo Zarra, katika Historia ya La Liga.

Dakika ya 92, Ronaldo alipiga Bao lake la 4 kwa Mechi hii na kuipa Real ushindi wa Bao 5-1.

La Liga itaendelea Jumatano Septemba 24,2014,Usiku ambapo Vinara, FC Barcelona, na Mabingwa Watetezi, Atletico Madrid, wote watakuwa Ugenini.

Jumatano Septemba 24,2014

2100 Rayo Vallecano v Athletic de Bilbao

2100 UD Almeria v Atletico de Madrid

2100 SD Eibar v Villarreal CF

2300 Malaga CF v FC Barcelona

2300 Sevilla FC v Real Sociedad

2300 Granada CF v Levante

Alhamisi Septemba 26,2014.

2100 RCD Espanyol v Getafe CF

2300 Valencia v Cordoba
 

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.

 

   Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad