KUHUSU BUNGE LA KATIBA TANZANIA:-Hii ndio Taswira ya Picha wakati Mbowe akitinga Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam Kuhojiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 18, 2014

KUHUSU BUNGE LA KATIBA TANZANIA:-Hii ndio Taswira ya Picha wakati Mbowe akitinga Makao Makuu ya Polisi Dar Es Salaam Kuhojiwa.

Waandishi wa habari wakirekodi  tukio la kuwasili kwa Mh. Freeman Mbowe (hayuko pichani) Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam leo Septemba 18,2014,alikoitwa kuhojiwa kuhusu kauli yake ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

 Mbowe alitoa kauli hiyo katika Mkutano Mkuu wa chama hicho Septemba 14, mwaka huu, akisema maandamano hayo yatafanyika katika siku ambayo itapangwa katika mikoa yote.

Siku moja baadaye, Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Kamishna Paulo Chagonja alimkemea akisema iwapo atafanya hivyo, hatua za kisheria zitachukuliwa.

 Pia, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) alimwandikia barua akimwita kuhojiwa.

Mh. Tundu Lissu akiwasili…Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Septemba 17,2014, kwamba uamuzi huo ni moja ya maazimio matatu ya kikao cha kwanza cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho iliyokutana Dar es Salaam.


Mbuge wa Ubungo, Mh. John Mnyika akiwa ndani ya gari baada ya kukataliwa kuingia.


Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mh.  Wenje (kushoto), Mh. Msigwa na Mh. Joseph Mbilinyi wakiingia katika jengo hilo.


Mwandishi wa habari Shamim Ausi mmoja wa wanahabari walioumia na kupoteza fedha na mali nyingine.


Wanachama wa Chadema wakiwa wamekalishwa chini na askari.


Kina Baba na Mama ambao ni wanachama wa Chadema waliofika makao makuu ya polisi.




Polisi wakiwakimbiza waandishi wa habari (hawako pichani) kwa kutumia mbwa.

Wanahabari wakiwa mekusanyika baada ya kutimuliwa na  mbwa.




Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi.


Muonekano wa polisi katika tukio hilo.


Askari wakiwa hawataki kuwaona wanahabari eneo hilo.


Mwandishi wa habari, Badi, akilia kwa uchungu baada ya kuumizwa na mbwa wa polisi.

MNYIKA, WANASHERIA WAZUIWA KUINGIA NDANI WANAHABARI WAKIMBIZWA NA MBWA, WAUMIA, WAMWAGA MACHOZI.

MAMIA  ya watu wamejitokeza leo Septemba 18,2014, kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam kuhusiana na kauli yake aliyotoa majuzi juu Septemba 16,2014 ya kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.

Kilichofuata ni Polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo  kwa umbali wa mita 200 ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao waliumia na kupoteza zana zao za kazi.

(Habari/Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad