MSHINDI WA MILIONI 50 ZA TMT 2014:-….Ni Mwanafaa kutoka Kanda ya Kusini,akiwa na Umri mdogo kuliko Washiriki wote. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 31, 2014

MSHINDI WA MILIONI 50 ZA TMT 2014:-….Ni Mwanafaa kutoka Kanda ya Kusini,akiwa na Umri mdogo kuliko Washiriki wote.

Mshindi wa milioni 50 za TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago.

Mshiriki kutoka Kanda ya Kusini, Mwanaafa Mwinzago amefanikiwa kuibuka kidedea na kutwaa shilingi milioni 50 za shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014.

Mwanaafa ambaye ndiye mshiriki aliyekuwa na umri mdogo kuliko wote ameshinda kitita hicho katika fainali iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Agosti 31,2014, Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
 
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo Agosti 31,2014, katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.

Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.

Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Agosti 31,2014,Katika Ukumbi wa Mlimani City.

Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.


Majaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014.

Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.


Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.


Malaika Band wakitoa Burudani wakati wa fainali ya TMT 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo Agosti 31,2014.

Christian Bella Akitoa burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo na Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi.

Joti akitoa Suprize ya ukweli haswa katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo Agosti 31,2014.


Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya MShindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) kupatikana na kila Mmoja kusherehekea Ushindi huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad