Mchungaji wa Kanisa la EAGT aliyetambulika kwa jina la Boniface Onesmo
alijikuta akibubujikwa na machozi mara baada ya kushuhudia mkewe Bi. Benta
Boniface akijifungua hirizi baada ya kushika mimba kwa kipindi cha miezi saba
na nusu.
Akizungumza na mtangazaji wa Kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm,
Edson Mkisi Jr, Mchungaji huyo alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mkewe
amekuwa na matatizo ya kuharibika kwa mimba za mara kwa mara na tangu kuhamia
kwa eneo hilo la Udingila Bagamoyo mkewe huyo hajawahi kuzaa mtoto hata mmoja
angawa amekuwa akishika mimba kila walipohitaji kuzaa.
“Kwa hakika Mungu ni mwema na sitaacha kuendelea kumsifu na kumuabudu,”
alianza kueleza Mchungaji Onesmo.
“Zaidi ya mtoto huyu mmoja niliyemzaa kabla ya kuhamia hapa, hivi sasa
kila ninapotaka kuzaa mtoto mimba za mke wangu zinaharibika na hadi muda huu
mimba zaidi ya nne zimeshaharibika nah ii nyingine ndio amezaa hirizi!”
Mchungaji Onesmo alisimulia.
Aliezeza kuwa siku ya tukio, mkewe kipenzi alianza kusikua uchungu tangu saa
nne asubuhi na kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo uchungu ulipozidi
kuongezeka.
“Hali iliendelea hivyo hadi saa nne usiku ambapo mkewe alihisi kabisa
kupushi na mimi nilikuwa tayari kumsaidia lakini wakati anaendelea kupushi
mkewangu akawa anatoa haja ndogo mara kwa mara na alitoa haja ndogo hadi ndoo
nne ndogo zilijaa na kumwaga nje.
“Baada ya hapo aliendelea kusikia maumivu makali ya tumboni huku akihisi
kuzaa lakini baadae aliposikia mtoto anakuja na mimi kujiweka tayari kumzalisha
niliona kitu kinatoka kama mtoto kukivuta ikatoka hirisi ikiwa imefungwa
kitambaa chenye rangi chekundu na nyeusi!” anasema.
Aidha, kwa upande wa mkewe, alisema kama siki hiyo kungekuwa na sumu ya
panya angekunywa afe akapumzike.
Akizungumze huku akilia, mama Dotto (Benta), anasema siku ya tukio hilo
roho yake ilinusa kaburi kama kama kungekuwa na hata mafuta ya taa kwenye kopo
angekunywa ili afe.
“Nilimuuliza mume wangu mara kadhaa kama kwenye kopo kuna mafuta ya taa
lakini aliniambia yote aliweka kwenye kandiri (taa ya chemli) na hata
nilipoangalia tunapoweka sumu sikuiona….kwa hakika kama ningekiona kimoja wapo
ningekunywa nife! Nimetesema sana,” anasema mama Dotto.
Mama Dotto alisema pamoja na changamoto zote anazokutana nazo Bagamoyo
lakini hajafikiria wala hafikirii kwenda kwa mganga wa kienyeji.
“Siwezi kwenda kwa mganga wa kienyeji kwa sababu waganga ukienda wao
huongeza tatizo kwa hiyo nitaendelea kumuomba Mungu hadi atakaposikia maombi
yangu,” anasema huku akiangalia na mumewe pamoja na majirani waliofika kumjulia
hali.
Akizungumza na Mkisi Jr, Mjumbe wa eneo hilo, Bw Hamza Adam, mbali na
kuthibitisha kufahamu kutokea kwa tukio hilo, pia alibainisha kwamba mbali na
tukio hilo ambalo hajawahi kukutana nalo tangu uhai wake, pia eneo hilo mifugo
imekuwa ikifa hovyo bila kuwepo kwa ugonjwa wowote.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
Like ukurasa wetu wa facebook ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Habari Na:-Times FM
No comments:
Post a Comment