LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Haya ndio matokeo ya Mechi za leo Agosti 30,2014 kwa Chelsea ikiibutua Everton 6-3, Manchester City na Manchester United wakishangazwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 30, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Haya ndio matokeo ya Mechi za leo Agosti 30,2014 kwa Chelsea ikiibutua Everton 6-3, Manchester City na Manchester United wakishangazwa.

Mabingwa wa Ligi kuu England msimu wa 2013/2014, Manchester City, Leo Agosti 30,2014,wamechapwa kwa Uwanja wa Etihad Bao 1-0.

 Bao la ushindi la Stoke limefungwa na Mchezaji wa zamani wa Man United, Mame Biram Diouf, katika Dakika ya 28 baada ya kukokota Mpira Mita 70 na kumzidi akili Kipa Joe Hart.

Huo ulikuwa ushindi wa kwanza wa Stoke dhidi ya City katika Mechi 12 za Ligi Kuu England Uwanjani Etihad na umekuja chini ya Meneja Mark Hughes ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man United na pia Meneja wa zamani wa City.

Nae Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (mbeke) akiwa na David Gill na Sir Bobby Charlton wakitazama mchezo wa timu hiyo leo Agosti 30,2014,ikilazimishwa sare ya 0-0 na Burnley. 

Man United imekuwa ikisuasua tangu kustaafu kwa Ferguson mwaka jana. Makocha wawili wamekwishapewa timu, David Moyes aliyetimuliwa mwishoni mwa msimu uliopita 2013/2014 na Ryan Giggs akakaimu kumalizia msimu, kabla ya msimu huu kuajiriwa Louis Van Gaal ambaye leo amefikisha mechi ya tatu bila ushindi, sare mbili ugenini, nyingine 1-1 na Sunderland na kufungwa moja nyumbani na Swansea City 2-1.  
Magoli 2 ndani ya Dakika 3 za kwanza ziliwapa Chelsea mwanzo mzuri Ugenini huko Goodison na Chelsea wakamaliza Mechi hii kwa ushindi wa Bao 6-3.

Bao hizo za mapema za Chelsea, zenye utata wa Ofsaidi, zilifungwa na Diego Costa na Ivanovic.

Everton walipata Bao lao la kwanza katika Dakia ya 45 kupitia Mirallas.
Hadi Mapumziko Chelsea 2 Everton 1.

Kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao la 3 mfungaji akiwa Coleman, alirjifunga mwenyewe, na Naismith kuipa Everton Dakika 2 baadae lakini Chelsea wakapiga Bao la Nne kupitia Matic na Dakika 2 baadae Mchezaji mpya wa Everton, Samuel Eto’o akaipigia Everton Bao la 3.

Huku Gemu ikiwa 4-3, Ramires akaipa Chelsea Bao la 5 katika Dakika ya 76 na Diego Costa akapiga Bao la 6 kuikata maini Everton.


Everton 3.

-Mirallas 45
-Naismith 69
-Eto'o 76

Chelsea 6.

-Diego Costa 1 & 90
-Ivanovic 3
-Coleman 67 [Kajifunga mwenyewe]
-Matic 74
-Ramires 77

Kesho Jumapili zipo Mechi mbili za Ligi Kuu England kati ya Aston Villa na Hull City na kufuatia ile ya Leicester v Arsenal


As It Stands Table EPL 2014/2015.


Position Team Played Goal Difference Points
Moving up 1 Chelsea 3 7 9
Moving up 2 Swansea 3 5 9
Moving down 3 Tottenham 2 5 6
Moving down 4 Man City 3 3 6
No movement 5 Arsenal 2 1 4
Moving up 6 Southampton 3 1 4
Moving down 7 Hull 2 1 4
Moving down 8 Aston Villa 2 1 4
Moving up 9 Stoke 3 0 4
Moving down 10 West Ham 3 -1 3
Moving down 11 Liverpool 2 -1 3
Moving up 12 QPR 3 -4 3
Moving down 13 Sunderland 3 -1 2
Moving down 14 Man Utd 3 -1 2
Moving up 15 Newcastle 3 -2 2
Moving down 16 Everton 3 -3 2
Moving down 17 West Brom 3 -3 2
Moving down 18 Leicester 2 -2 1
Moving down 19 Crystal Palace 3 -3 1
Moving down 20 Burnley 3 -3 1
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad