Rais Kikwete
akiwahutubia wananchi toka nchi za Burundi na Tanzania waliofurika katika mpaka
wa Mugikomero alisema mpaka umeimarishwa
siyo kwasababu kuna mgogoro bali ni kutokana na ushirikiano na mahusiano mazuri
kati ya wananchi wa Tanzania na Burundi.
“Ni vyema
kuimarisha mipaka yetu kusudi wananchi waelewe wapo upande gani wa nchi hizi
mbili ili kuweka mahusiano mazuri na kuondoa mkanganyiko ni wapi baadhi ya
wananchi wanatoka, baada ya kuimarisha mipaka wao wenyewe wataona na kujua ni
raia wan chi gani. Alisema Rais Kikwete.
Rais kikwete
alisema kuwa uimarishwaji wa mpaka kati ya Tanzania na Burundi ni agizo la
Umoja wa Nchi za Afrika (AU) ambapo Umoja wa nchi za Afrika uliagiza nchi
wanachama ifikapo mwaka 2017 nchi zote ziwe zimeimarisha mipaka yao kwa
makubaliano ili kuondoa migogoro kati ya nchi moja na nyingine isiyokuwa ya
lazima.
Mara baada
ya mpaka wote wa Tanzania na Burundi kuwa umeimarishwa utasainiwa mkataba wa
makubaliano kati ya Tanzania na Burundi na kuufuta mkataba wa mipaka uliowekwa
na wakoloni na mkataba huo utakuwa wa Watanzania na Warundi na siyo Waingereza
na Wajerumani.
Rais Kikwete
alisistiza kuwa kwa kizazi cha sasa kilichoshuhudia kazi za kurudisha mawe ya
mipaka kitakuwa mlinzi wa mpaka na anaamini kuwa mawe ya mipaka hayawezi
kuhujumiwa wala kung’olewa kwani sasa wananchi wameelewa nini maana ya mawe
hayo na wataendelea kuyalinda na kudumisha udugu kati ya nchi mbili.
“Marafiki
huchora mipaka kwa kalamu kukiwa na amani na utulivu lakini maadui huchora
mipaka kwa nguvu na wino wa damu sisi ni ndugu na mipaka yetu tumeimarisha kwa
makubaliano makubwa na ushirikiano na tutaendelea kudumisha amani na utulivu
daima” Alisistiza Rais Kikwete.
|
No comments:
Post a Comment