AJALI/MVUA:-Picha 10 za mawe ya Mwanza yalivyoporomoka na kuua ndugu zetu wanne. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, August 19, 2014

AJALI/MVUA:-Picha 10 za mawe ya Mwanza yalivyoporomoka na kuua ndugu zetu wanne.


Huko Jijini Mwanza, athari za watu walivyojenga pembeni au karibu ya mawe makubwa milimani zimeanza kujitokeza ambapo Kwenye kumbukumbu zangu sikumbuki kama niliwahi kusikia kuporomoka kwa haya mawe lakini kama Bindamu niliwahi kuwa na hofu hiyo.

Natoa pole sana kwa ndugu waliopoteza ndugu zao wanne baada ya mvua kunyesha usiku wa kuamkia  Agosti 17,2014 kisha nyumba zao kuporomokewa na haya mawe makubwa maeneo ya Mabatini Sinai mtaa wa Nyerere A Jijini Mwanza.








WATU wanne wa familia mbili tofauti, wamepoteza maisha huku wengine wawili wakijeruhiwa katika eneo la Sinai-Mabatini, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza baada ya kuporomokewa na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na radi usiku wa kuamkia  Agosti 17,2014.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentine Mlowola, tukio hilo lilitokea saa 8:55 usiku, ambapo mvua kumbwa iliyoambatana na upepo wa wastani na radi nyingi ilinyesha na kusababisha majabali makubwa ya mawe yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani mbili kuporomoka na kuziponda nyumba hizo.

Aliwataja waliokufa kuwa ni wanafunzi wawili wa shule ya msingi Mbugani, Kefa Joseph (15) na Emmanuel Joseph (12) kutoka katika familia ya Joseph William yenye watu watano, huku mtoto Godfrey Joseph akijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.

Kamanda aliitaja familia nyingine iliyoathirika kuwa ni ile ya Samson Odinya ambaye alifariki pamoja na mkewe Kwinta Geko (24) huku mtoto wao, Betty Samson (4) akijeruhiwa.

Tanzania Daima lilifika eneo hilo, saa mbili asubuhi na kuushuhudia nyumba hizo zikiwa zimesambaratishwa kabisa huku nyingine iliyo jirani jiwe likiwa limejikita katikati.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya majirani lisema kuwa nyumba zilizofikwa na maafa zinamilikiwa na Joseph William na Lameck Ajiji.

Tukio hilo lilivuta lilivuta hisia za wakazi wengi wa jiji la Mwanza huku wengine wakishindwa kujizuia na kuangua vilio.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), alifika eneo la tukio kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoathirika na janga hilo, ambapo alionesha kushtuka baada ya kuelezwa na wananchi kwamba hakuna kiongozi yeyote wa serikali aliyekuwa amefika eneo hilo.

Akizungumza mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika katika eneo hilo, Wenje alisema; “Inashangaza sana kuona hata mkuu wa wilaya hajafika hapa. Nitawasiliana na viongozi wa serikali na mchana nitarudi hapa tena.”

Mmoja wa wananchi hao, ambaye ni Balozi wa shina namba 5 Mtaa wa Nyerere A, Jackson Kitundu alisema kuwa tukio hilo linasikitisha sana, na kwamba wanaomba viongozi wa serikali wasaidie kuwaondoa wananchi  kwenye maeneo ya miamba.


Picha Na:- http://millardayo.com
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WhatsApp:- 0789-925-630.
 Like ukurasa wetu wa facebook  ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad