...Aliyekatwa
nyembe miaka 21.. katika Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa, lilitokea Julai
5,2014 saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B mkoani Morogoro.
|
Stori:
Dustan Shekidele, Morogoro.
MWANAMKE
mmoja, Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa
mtu, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata ya Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro
amechanwa na nyembe mwilini na baadaye kutembezwa bila nguo mtaani mchana
kweupe akituhumiwa kufumwa na mume wa mtu.
Tukio hilo
la aina yake ambalo lilivuta umati
mkubwa, lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B.
Mashuhuda wa
tukio hilo walipohojiwa na mwandishi wetu walidai kuwa kwa muda mrefu, Zaitun
Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu Rehema akidai
anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego bila mafanikio.
“Zaituni
baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita Rehema nyumbani kwake na kudai
amewafuma na mumewe hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo na kumtembeza
bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300 mchana kweupe,” alisema
mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Ally.
............Rehema
Juma akiwa na Mama yake..................
|
Mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Rehema na kumkuta akiwa amefungwa bendeji sehemu za mwili wake na alipoulizwa alifafanua:-....
“Ni kweli
tukio hilo limetokea lakini siwezi kuzunguma peke yangu, twende kwa mama mkwe
Mtaa wa Ngerengere.”
Mwandishi
wetu na Rehema walipofika kwa mkwe wa mtuhumiwa, Lilian Julius Sechonge ambaye
ni mjumbe wa serikali za mtaa wa Ngerengere na kutakiwa kuzungumzia tukio hilo
alikuwa na haya ya kusema:-........''
.....Mtuhumiwa
wa tukio hilo....... Zaitun
Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu Rehema akidai
anatembea na Mumewe......
|
“Ni kweli Rehema ni mkwe wangu kwa mwanangu aitwaye Godfrey Sechonge anayeishi naye hadi sasa, Julai 5, mwaka huu mwanangu huyo alikuja na akaniambia mkewe anatembezwa bila nguo.
“Nilifika
eneo la tukio na kumkuta mkwe wangu yuko uchi huku akivuja damu mwili mzima.
“Aliniambia
amecharangwa viwembe na Zaituni akimshutumu kutembea na mumewe, nilimchukua
mwanangu na kumkimbiza polisi ambapo tulipewa PF3 na kufunguliwa jalada namba
MOR/RB/4009/2014.”
Naye Rehema
alipozungumzia kisa hicho alisema siku ya tukio saa 4 asubuhi, Zaituni alimtuma
mwanaye nyumbani kwake na kumuomba aende kwake (Zaituni).
“Nilipofika
kwake aliniingiza ndani na kuniwekea kisu shingoni huku mwanaye akinirekodi na
simu yake, akaniuliza nimetembea mara ngapi na mumewe!
“Alitaka
kujua pia amenihonga shilingi ngapi, kwa hofu ya kuchinjwa nilikubali kwamba
nilitembea naye mara moja na alinipa shilingi elfu tano. “Baada ya kusema hivyo
akaniachia, nikarudi nyumbani.
Saa kumi
aliniita tena, nilipofika nikamkuta yuko na mumewe na watoto wao, akaniuliza
unamjua huyu? Nikamwambia simjui, akatoa simu na kufungua mahojiano, mumewe
alipojaribu kumpora, akamchanja na wembe.
.............Mtuhumiwa
akihojiwa...............
|
“Ghafla
akahamia kwangu na kuanza kunichanja kwa wembe huku nikipiga kelele na akanivua
nguo kisha akanitoa nje na kunipeleka kwangu nikiwa na nguo ya ndani tu,”
alisema Rehama.
Akizungumza
na mwandishi wetu,diwani wa kata hiyo, Lydia Mbihaji alisema tangu aanze
kuongoza watu hajawahi kukutana na tukio kama hilo ambalo aliliita ni la
kinyama.
Tayari
Rehema amelifikisha sakata hilo polisi na Zaituni alikamatwa na kuwekewa
dhamana na Mumewe akisubiri kuburuzwa mahakamani wakati wowote.
Baada ya
kudhaminiwa, mwandishi wetu aliwashuhudia Zaituni na Mumewe wakizungumza na
Rehema ambapo inadaiwa wanataka ipatikane suluhu kabla kesi haijaanza
kuunguruma Mahakamani.
No comments:
Post a Comment