JINAMIZI LA KUJITOA UHAI-NGARA:-Wanaume wawili wafa wilayani Ngara,mkoani Kagera kwa Kujinyonga mmoja akitumia Kitenge na mwingine mkanda wake wa Suruali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 15, 2014

JINAMIZI LA KUJITOA UHAI-NGARA:-Wanaume wawili wafa wilayani Ngara,mkoani Kagera kwa Kujinyonga mmoja akitumia Kitenge na mwingine mkanda wake wa Suruali.


Muonekano wa mwili wa  Godwin Yustus  mkazi wa kijiji cha Mkirehe wilayani Ngara mkoani Kagera , mwenye umri wa miaka 48  ukiwa umening’inia baada ya kujinyonga kwa kitenge  na kujininginiza juu ya mti wa mwembe  nyuma ya nyumba yake jana(Julai 14,2014) majira ya saa kumi na mbili jioni.


Tukio la kugundulika kwa Mwili huu juu ya Mwembe lilibainika na Mtoto wake wa mwisho wa Marehemu,  Elastoni Godwini  wakati akienda kubembea na Marafiki zake kwenye mti huo ambao huutumia  kubembea.
 


Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera FM-Ngara,Kanyesha Faustine(kulia) alifanya mahojiano na Mke wa marehemu Bi Elisa Godwin  na kusema kuwa Mumewe alikuwa na hali ya kuchanganyikiwa  na kuzungumza maneno/vitu ambavyo  walikuwa wanashindwa kuelewa  na kudai kuwa henda hali hiyo ndiyo imemsababisha yeye kujinyonga.

Amesema tangu siku ya Jumanne  ya wiki iliyopita marehemu  alikuwa  akidai kuwa kuna watu ambao walikuwa wanataka kumchoma moto  na hivyo  kwenda kushitaki kituo cha Polisi .

Bi Godwni amedai kuwa marehemu  siku ya Jumamosi(Julai 12,2014)  alipotea nyumbani na hawakujua ni wapi amekwenda na  hivyo kuripoti kwa Uongozi wa Serikali ya kijiji na siku ya Jumapili (Julai 13,2014) asubuhi  alifika nyumbani na hawakujua ni wapi ametokea.


Wanakijiji  wakiwa Msibani .....ambapo Mtendaji wa kijiji cha Mkirehe Bw. Zacharia Kahozi amekiri kuwa  familia ya marehemu imekuwa ikija kuripoti  juu ya hali ya marehemu katika ofisi za kijiji hicho kuhusu kuchomwa moto na watu wasioonekana hali iliyowafanya wahisi kachang'anyikiwa akili.



.......Kaburi ambalo litatumika kuuzika mwili  wa marehemu ......


Katika tukio Jingine ,Mkazi wa kitongoji cha  Mbinyange Wilayani Ngara Mkoaani Kagera ,Hakiza Biroha mwenye umri wa miaka 36 amekutwa amejinyonga kwa kutumia  mkanda wa suruwali katika kijiji cha Chivu kitongoji cha Mgwabila ,Kata ya Ntobeye wilayani humo.

Jeshi la Polisi limesema kuwa Marehemu aliondoka nyumbani kwake Julai 09,2014,majira ya saa Nane akiwa na fedha shilingi Elfu 40 na Baiskeli yake ,akidai kuelekea katika shughuli zake za uuzaji wa Mayai ambapo siku iliyofuata ya Julai 10,2014,mwili wake ulikutwa chini ya mti ukiwa tayari umefariki kwa kujinyonga akitumia mkanda wa suruali yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad