AJALI :-Tazama Picha ya Ajali ya Magari mawili na Pikipiki ikiua Watu watatu mkoani Arusha. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 15, 2014

AJALI :-Tazama Picha ya Ajali ya Magari mawili na Pikipiki ikiua Watu watatu mkoani Arusha.


Gari aina ya Range Rover lenye namba T 961 ARC  likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Corolla katika ajali iliyotokea katika makutano ya barabara kuu ya Moshi/Arusha na ile ya kuelekea ofisi za mkuuu wa wilaya ya Moshi na kuua watu watatu..Picha Na:-Dj sek Blog.



Gari aina ya Range Rover lenye namba T 961 ARC likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo



Gari dogo aina ya Toyota Corolla lilikiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Range Rover katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi jirani kabisa na kipita shoto(Keep left) cha Arusha.


Mifuko maalumu ya kuzuia abiria asiumie wakati wa ajali ikiwa imefumuka baada ya ajali .



Pikipiki ikiwa chini ya uvungu wa gari aina ya Range Rover baada ya kugongwa katika ajali iliyotokea katika makutano ya barabara kuu ya Moshi/Arusha na ile ya kuelekea ofisi za mkuuu wa wilaya ya Moshi.



Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakitizama pikipiki iliyokuwa chini ya uvungu wa gari hiyo.


Hivi ndivyo pikipiki inavyoonekana ikiwa chini ya Uvungu wa gari.


Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakichukua vipimo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambayo watu wawili wanadaiwa kufariki dunia papo hapo huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya akiwemo dereva bodaboda aliyevunjika miguu.


Baadhi ya wananchi wakitizama ajali iliyotokea katika makutano ya barabara kuu ya Moshi/Arusha na ile ya kuelekea ofisi za mkuuu wa wilaya ya Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad