![]() |
|
Kila mmoja
wetu kwa wakati fulani huhisi kuvimbiwa na gesi nyingi tumboni…..Suluhu ya
pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni.
|
Wanayansi
katika chuo kikuu cha Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu
mbaya kama vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa
afya ya binadamu.
Wanasayansi
hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya
moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au
harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza
kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Utafiti huo
uliochapishwa katika mtandao wa chuo kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo
inayojulikana kama Hydrogen Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai
yaliyooza, inaweza kuwa muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"Ingawa
gesi ya hydrogen sulfide inajulikana kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika
Mayai yaliyooza pamoja na harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na
inawezekana kuwa tiba kwa magonjwa fulani,'' anasema Daktari Mark Wood,Profesa
wa chuo hicho cha Exeter.
Gesi hiyo
ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Chanzo:- BBC
Swahili.






No comments:
Post a Comment