Kanisa kuu
la Anglikana Uingereza ambapo Baraza kuu la kanisa la Kianglikana
Uingereza, The General Synod, limeidhinisha Wanawake kuwa maaskofu.
|
Maafisa
katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo.
Sasa baada
ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa
kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Makasisi
wanawake walio thuluthi moja ya viongozi wa kidini wa kanisa la kianglikana,
wanasema haki sawa itawapandisha hadhi katika makanisa.
Hatua hiyo
inemaliza mvutano wa miaka mingi na kuvunja utamaduni wa makarne katika kanisa
hilo. Tofauti nyingi zimeibuka kuhusu suala hilo na hata kusababisha
migawanyiko katika kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi yameshawatawaza
maaskofu wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la kanisa kuu.
Nchi zilizo
na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini.
'Msimamo
wa viongozi wa kanisa hilo Afrika'
Kasisi Moses
Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda ameambia BBC kuwa misimamo
imegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na mafundisho ya Bibilia.
''Kanisa la
Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi limechukua msimamo
wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono'' amesema kasisi Bushendich.
Baadhi ya
itikadi ambazo zimekuwepo kwa miaka m ingi katika makanisa kuu kama vile
Katoliki na Anglikana ni wanawake kuwa maaskofu wanawake, na kruhusu ndoa ya
wapenzi wa Jinsia moja ambayo tayari baadhi ya maumini na maaskofu wa kanisa
hilo wamepigia debe kuidhinishwa.
Habari Na:-BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment