Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kinaamini kilishinda uchaguzi
wa Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 chini ya mfumo wa vyama vingi.
Katibu Mkuu
wa CHADEMA, Dk Willbrod Slaa, ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya
chama hicho kwenye uchaguzi huo, alibainisha hayo hivi karibuni wakati wa
mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili.
Dk Slaa
alisema kuwa ana uhakika kuwa chama chake kilipata kura nyingi zaidi za urais,
tofauti na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Mrisho Kikwete
aliyetangazwa mshindi
.
“…Baada ya
uchaguzi wa mwaka 2010, tulikataa kumtambua Rais Kikwete, ingawa wakati ule
hatukujua kwa uhakika kama tulishinda. Kadiri nilivyozunguka, ndiyo kadiri
tulivyoanza kuamini kwamba tulishinda,” alisema Dk Slaa.
Alisema kuwa
takwimu walizonazo zinaiaminisha Chadema kwamba ilishinda Uchaguzi Mkuu wa
urais mwaka 2010.
“Sababu,
unafika kwenye jimbo wanakusomea kura ulizopata katika uchaguzi ule
wakizilinganisha na alizozipata Kikwete na Profesa Ibrahim Lipumba… wanasema
Dokta hapa ulimshinda… kwa kura 20,000, pale ulimshinda kwa kura 15,000 pale
ulimshinda kwa kura…,” alifafanua na kusisitiza:
“Sasa ndiyo,
tuna uhakika kama tulishinda na ndiyo maana Kikwete hajawahi kwenda kwa
wananchi kushukuru kwa kumchagua, tofauti na tabia yake. Anachofanya sasa ni
kwenda kuzindua miradi.”
Hata hivyo,
Dk Slaa alisema hawakuweza kuendelea na madai yoyote kwa sababu kwa mujibu wa
Sheria na Katiba ya nchi, mshindi wa urais akishatangazwa hairuhusiwi kupinga
kwa namna yoyote hata mahakamani, akieleza kuwa hiyo pia ndiyo sababu ya
kuhitaji Katiba Mpya.
Habari Na:-Mwananchi.
No comments:
Post a Comment