UFISADI NGARA:-Baraza la Madiwani Ngara lamtaka Mkurugenzi Kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Meneja wa Mamlaka ya Maji kwa ubadhirifu wa Fedha JK. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 25, 2014

UFISADI NGARA:-Baraza la Madiwani Ngara lamtaka Mkurugenzi Kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Meneja wa Mamlaka ya Maji kwa ubadhirifu wa Fedha JK.


Rais Kikwete akihutubia wananchi kijiji cha Rulenge, Ngara mkoani Kagera katika mkutano wake alioufanya kijijini hapo Julai 27,2013. (Picha zote na Maktaba Yetu)



Rais Kikwete akiwasilimia wananchi wa Ngara, mkoani Kagera wakati wa ziara yake Julai 27,2013,mjini humo.

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani  Kagera  limemtaka Mkurungezi wa Halmashauri hiyo kumpeleka Mahakamani  aliyekuwa Meneja wa Mamlaka ya maji safi na mazingira wilayani  Ngara,  ambaye  alistafu mwaka huu Bw Edward  Magai  baada ya kubainika  kufanya ubadhilifu wa fedha zilizotumwa na  Rais Jakaya Kikwete Milioni Mia moja na 50  kwa ajili ya kutatua kero ya mji mjini Ngara.

Baraza hilo la Madiwani limemetoa  mapendekezo hayo leo(Julai 25,2014)  katika kikao cha Madiwani kilichofanyika  katika ukumbi wa halmshauri  ya wilaya hiyo baada ya kupokea  taarifa za  kamati ya Mipango na Fedha iliyowasilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Bw Sudi Mkubila. 

Kutokana na taarifa  hiyo ya ubadhilifu wa fedha za Rais  Kikwete  alizoztoa  baada ya kupata kilio cha wakazi wa mji wa Ngara  mwaka jana , baadhi ya madiwani wakichangia hoja hiyo,wametaka Meneja huyo Mstaafu achukuliwe hatua za kisheria kwani alikiuka maagizo ya Rais kuhusu matumizi ya fedha hizo.

Kwa upande  wake mkurugenzi  wa halmashauri ya Wilaya ya Ngara ,Bw .Corlonel  Ngudungi  amesema kuwa fedha hizo milioni Mia moja na 50 ziliingia kwenye akaunti ya Mamalaka  ambapo  alikiuka maelekezo aliyoagizwa kuyafuata.  

Baada ya  kupokea  taarifa hiyo,Baraza limekaa kama kamati  na kumchagua Bw Matiasi Mugata  kutoa taarifa zilizopitiwa na mkaguzi wa ndani  na kubaini kuwa  mtumishi huyo  mstafu wa mamalaka ya maji  safi na mazingira  Bw Edward Magai alifanya ubadhifu wa fedha zilizotolewa na Rais Kikwete  kwa ajili ya kusaidia kupunguza kero ya maji mjini Ngara ,afikishwe mahakamani kwani ni aibu kuiba fedha za Rais.

Fedha zilizobainika kuibiwa  ni Shilingi  Milioni 30, laki 6 na 47 elfu mia 8 themanini na sita na senti 93 .

Kwa Upande wake,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara,Bw.Hadson Bagege amewapongeza Madiwani kwa kuonyesha ukomavu na kuisimamia halmashauri hiyo  hali iliyosababisha  kupata hati safi licha ya mapungufu yaliyobainishwa kwenye ripoti ya mkaguzi  na mdhibiti mkuu  wa hesabu za serikali CAG.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad