Ni muonekano wa Mlima/Pori ambalo lilikutwa limechomwa moto na Watuwasiojulikana katika Kijiji cha Kasharaji wilayani Ngara mkoani Kagera huku juhudi za kudhibiti uchomaji moto hovyo unaoharibu Mazingira na hata Kuharibu Miti iliyopandwa katika Viwanja likisuasua.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Bw Cornel Ngudungi amesema
mapendekezo kuhusu kugawanywa kwa Jimbo la uchaguzi la Ngara yatatolewa kwenye
kikao kijacho cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Bw Ngudungi
ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akijibu swali la diwani wa Kata ya Bugarama Bw
Adroniz Bulindoli wakati wa maswali ya Papo kwa Papo katika kikao cha Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ngar.
Amesema
suala hilo tayari limejadiliwa kwenye kikao cha CMT na kwamba mapendekezo ya
kugawanya Jimbo hilo la uchaguzi yatatolewa rasmi kwenye kikao kijacho cha
Baraza la Madiwani.
Awali Bw
Bulindoli ameshauri Jimbo la Uchaguzi la Ngara ligawanywe ili yapatikane
majimbo mawili ambayo ni Ngara Kusini na Ngara Kaskazini kwa lengo la kusogeza
huduma karibu na wananchi kutokana na ukubwa wa Jimbo la sasa pamoja na idadi
ya watu waliopo.
Habari Na:-Radio Kwizera-Ngara.
|
No comments:
Post a Comment