Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Jafari Kasisiko , Katibu wa mkoa Msafiri Wamalwa na Katibu wa Baraza la wanawake, Bi. Malunga Simba wa chama hicho Mkoa wa Kigoma wametangaza kujizulu nafasi zao na uanachama wa chama hicho na kuachia nyadhifa zao kuanzia Julai 18,2014 .
Akitangaza
uamuzi huo kwa niaba ya wenzake mbele ya waandishi wa habari mkoani Kigoma,
Mwenyekiti Jafari Kasisiko, amesema yeye na wenzake wamefikia uamuzi huo
baada ya kuona kuwa CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama cha kidemokrasia na
kuwa chama cha kibabe.
“Sifa kubwa
ambayo ilikuwa imetufanya tuendelee kubakia Chadema ni kwamba kilikuwa bado
kinaendelea na sifa ya kuwa ni chama cha kidemokrasia, lakini baada ya kufikia
hatua sasa kwamba kimeanza kuwa chama cha kibabe zaidi na kuanza kukiuka
misingi ya demokrasia, kwa kweli sina sababu na wenzangu ya kuendelea kubaki
katika chama hichi,”alisema.
Mzee
Kasisiko ambaye aliondoka CCM mnamo mwaka 1985 na kukaa nje ya siasa kwa muda
kabla ya kujiunga Chadema mwaka 1994, alitoa mfano unaoonesha CHADEMA, kukiuka
misingi ya demokrasia kuwa ni suala la aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama
hicho, Zitto Kabwe, ambaye alivuliwa wadhifa wake kufuatia kutangaza nia ya
kutaka kugombea moja ya nafasi za juu ndani ya chama hicho.
“Mheshimiwa
Zitto, kosa lake pekee ni kwa sababu alionesha nia ya kutaka kugombea uenyekiti
wa Chadema. Lakini ukipitia katiba ya Chadema tangu ukurasa wa kwanza mpaka wa
mwisho, hupati mahala panaposema ni kosa mtu kutamani kugombea nafasi yoyote
katika chama.”
“Yeye
kuonekana kuwa alikuwa na nia ya kutaka kugombea, na kikubwa zaidi tayari
alikuwa na watu wanaoumuunga mkono, na mimi nikiwa mmoja wao, basi hili
lionekana ni dhambi kubwa sana.”
“Kwa hiyo
katika Chadema tulikuja kugundua kwamba kumbe uenyekiti sasa hivi, ukiacha
uenyekiti wa zama za Mtei, uenyekiti zama za Makani lakini uenyekiti chini ya
mheshimiwa Mbowe ni kitu nyeti ambacho hatakiwi mtu mwingine kugusa.”
“Kwa hiyo
kitendo hichi kwetu sisi kilionesha wazi kuwa Chadema wamefikia mahala sasa
hawako tayari kufuata taratibu za kidemokrasia.”
Alisema
pamoja na kwamba na wamechukua muda mrefu kabla ya kutangaza uamuzi huo
walikuwa na sababu za msingi ambazo ziliwafanya wasitangaze, lakini tangu siku
Zitto Kabwe alipovuliwa nyadhifa zake walikuwa hawana imani tena na chama kwa
sababu hawawezi kuwa ndani ya chama ambacho ni mamlaka ya watu Fulani.
Kwa upande
wake Msafiri Wamalwa alisema kwa ridhaa yake bila kushawishiwa na mtu ameamua
kuondoka Chadema na kwamba kabla ya uamuzi huo alikaa chini na kutafakari,
wakati Malunga Simba alisema ameamua kutoka Chadema kwa sababu ni chama ambacho
hakina faida na wananchi.
Baada ya
kujiuzulu uongozi na uanachama wa Chadema, Mzee Ramadhani Kasisiko alisema
anajiunga na chama kipya cha siasa cha Allience for Change and Transparency,
ACT, lakini wenzake hawakuzungumzia kama kuna chama wanachohamia ingawa
Msafiri Wamalwa alisema atatafuta chama makini.
No comments:
Post a Comment