MATOKEO MAKUBWA SASA-NGARA:-Taswira ya Vyoo vinavyotumika na Wanafunzi wa Shule ya Msingi iliyobeba Jina la Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ngara-Ngeze shule ya Msingi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 14, 2014

MATOKEO MAKUBWA SASA-NGARA:-Taswira ya Vyoo vinavyotumika na Wanafunzi wa Shule ya Msingi iliyobeba Jina la Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ngara-Ngeze shule ya Msingi.


Ni muonekano wa Vyoo vianavyotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ngeze iliyopop kata ya Muganza wilayani Ngara mkoani Kagera.

 Vyoo hivyo vinaelezwa kuwa si bora kwa matumizi ya Wanafunzi hao kwa sababu sakafu yake ni miti iliyopangwa bila kufunikwa na ni hatari Kiafya  kwa watumiaji.


Changamoto hii ya Kuwa na Vyoo bora katika Makazi pia hata kwa Baadhi ya Shule zetu Nchini Tanzania linatajwa na Waziri  wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Tanzania,Dkt. Seif Rashid (MB) Kwamba ni asilimia 29.6  hazina vyoo kabisa huku asilimia 9 kuna vifaa maalum kwa ajili ya kunawa mikono jambo ambalo ni hatari kubwa kwa afya kutokana na wananchi wengi kuwa na mwitikio mdogo wa kujenga vyoo  bora vya kisasa.

Wizara yake ilifanya utafiti katika Halmashauri 112 nchini mwaka 2013 ambapo matokeo yanaonyesha asilimia 25 tu ya Kaya kutumia vyoo bora.


Baada ya kufanyiwa Marekebisho,Vyoo hivyo Vya shule ya Msingi Ngeze huonekana kwa taswira hii.


.....Tazama Muonekano wa sakafu kwa baadhi ya Vyoo hivi......Sipati picha  Mtoto akiteleza inakuwaje ....kama si Majanga ...??.


Hiki inasemekana kinatumiwa na Walimu wao wa Shule ya Msingi Ngeze na kwa nyuma ni Vyoo vya Wanafunzi.


Shule hii ya Msingi iliyobeba jina la aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara,mkoani Kagera kimadarasa yanaonekana yako katika hali nzuri na inayo Madarasa 7.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad