AJALI NGARA/PICHA:-Furaha ya Ujerumani kuwa Bingwa wa Kombe la Dunia 2014-Yasababisha Ajali ya gari dogo kuivaa Nyumba Mjini Ngara… - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 14, 2014

AJALI NGARA/PICHA:-Furaha ya Ujerumani kuwa Bingwa wa Kombe la Dunia 2014-Yasababisha Ajali ya gari dogo kuivaa Nyumba Mjini Ngara…


Kwa haraka haraka unaweza sema imepaki…kumbe ni ajali ya Gari Namba T 500 CWC iliyotokea Jana Julai 13,2014,Usiku was aa 8 katika Barabara ya kuelekea Hospitali ya Murgwanza mjini Ngara.


Inaelezwa chanzo cha Ajali hiyo huenda imesababishwa na Ulevi uliopindukia kwa Dereva wake ambaye alikuwa akitoka kutazama Fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa Ujerumani kuibuka Bingwa kwa kumfunga Argentina bao 1-0.


Mashuhuda wa tukiohilo wanaeleza kuwa ..Dereva wake ambae jina halikujulikana mara moja,akiwa kapiga Pombe kisawasawa alianza safari ya kuelekea Murgwanza ambapo katikati ya safari hiyo ghafla alishindwa kulimudu gari lake hilo  na kuivaa Nyumba ya Kaka mmoja ajulikanae kwa jina la ZONGO ambaye alikuwa staff wa Benki ya NMB Tawi la Ngara ,kwa sasa kahamishwa kikazi.


Katika ajali hiyo haijajulikana ni watu wangapi walikuwemo ila hakuna mtu aliefariki ,zaidi ya Kupatikana Majeruhi ambao walipelekwa Hospitali ya Murgwanza kwa Matibabu Zaidi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad