Bi. Nasra
Ally kutoka Nairobi Kenya akiwa katika maonesho ya sabasaba katika manispaa ya
Bukoba mkoani Kagera.
|
Wafanyabiashara
kutoka nchini Kenya waliohudhuria maonesho ya sabasaba katika maispaa ya Bukoba
mkoani Kagera wameitaka jumuia ya afrika ya Mashariki kuondoa vikwazo katika
mipaka ya nchi wanachama ili kutoa fursa za masoko kwa jumuia hiyo
Mkurugenzi
wa Shirika linalojihusisha kukuza maendeleo ya kilimo na
Biashara mkoani Kagera (KAIDEP) Bw Philmon Kamazima amesema katika
washiriki hao ni kutoka katika mashirika , makampuni na taasisi
mbalimbali za uzalishaji mali.
Bw Kamazima
amesema kuwa kati ya wa washiriki hao 203 ni kutoka hapa nchini na 59 wametokea
nchi za Uganda Kenya na Rwanda ambapo amesema katika maonesho hayo wanasisitiza
ubora wa bidhaa na upanuaji wa masoko kimataifa.
Amesema
katika ukuzaji wa uchumi kwa wananchi walioko katika jumuia ya
Afrika Mashariki ni bora walio na makampuni na wafanya biashara wakubwa
kuwekeza bidhaa zao na kupata sokola pamoja ili kuongeza uzalishaji wa
bidhaa .
No comments:
Post a Comment