WAANDISHI WANAPOKUTANA:-Mkutano Mkuu wa Kagera Press Club katika Picha - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 05, 2014

WAANDISHI WANAPOKUTANA:-Mkutano Mkuu wa Kagera Press Club katika Picha

Wanachama wa Kagera Press Club, Ashura Jumapili na Ayoub Mpanja wakijibu hoja kwa wanachama baada ya Kamati ya Shida na Raha wanayoiongoza kushindwa kutekeleza majukumu yake,wakati wa Mkutano mkuu wa KPC uliofanyika Julai 04,2014 katika Ukumbi wa Lake Hotel mjini Bukoba.

Prudence Kibuka akitetea Kamati ya Miradi ambayo pia yeye ni mjumbe.

Wanachama wakifuatilia Mkutano huo mkuu wa KPC uliofanyika Julai 04,2014 katika Ukumbi wa Lake Hotel mjini Bukoba.

Antidius Kalunde akitoa hoja ya kupigwa'stop'kwa watu wanaodai ni waandishi wa habari ambao hutoka vyuoni na hupiga kambi ofisini bila uthibitisho wowote..Picha Na:-Harakati News.

Ramadhani Makonda ambaye ni Mwanachama na Mtangazaji wa Redio Kwizera na mmiliki wa Blog ya Mwanawamakonda akichangia hoja baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utekelezaji kwa mwaka 2013/2014.

Pontian Kaiza akilaumu kuwa anawekewa vikwazo katika utaratibu wa kuazima vitendea kazi.

Pamoja na kupata Taarifa mbalimbali za Utekelezaji kwa mwaka 2013/2014,mkutano huo mkuu wa KPC ulishindwa kupitisha Wanachama 13 wapya walioomba kujiunga kutokana na Kamati tendaji kushindwa kukutana  kupitia Majina na kuyatangaza UBAONI  kwa Mujibu wa Katiba Kabla ya Mkutano mkuu kufanyika ili kuwapitisha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad