Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova akitoa taarifa kwa wanahabari jana Julai 22,2014.
|
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum la Dar es Salaam linawashikilia watu nane na kuwahoji
kuhusu tukio la kupatikana kwa viungo vya binadamu vilivyogundulika katika
maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, Bunju B Julai 21, mwaka huu ambapo mifuko ya
plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu iligundulika.
Polisi
walipata taarifa za tuki hilo kutoka kwa wasamaria wema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, polisi walipofika eneo la tukio waligundua mifuko ipatayo 85 yenye viungo vya binadamu vilivyokaushwa na kukakamaa vikiwemo vichwa, miguu, mikono, mioyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu.
Katika eneo
hilo, pia vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa
mikononi (gloves) mifuko miwili iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na
karatasi mbili zenye maswali ya kujibu.
Moja ya kichwa cha Binadamu ambacho kimetolewa
katika moja ya Mifuko hiyo.
|
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo
inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili ya Binadamu.
|
Baada ya tukio hilo, viungo hivyo vilichukuliwa na kupelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Baada ya
uchunguzi wa kina imebainika kuwa viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa
katika Maabara ya Chuo Kikuu cha Madaktari IMTU jijini Dar es Salaam na hivyo polisi
wamewakamata na sasa wanaendelea kuwahoji watu nane ambao wanasadikiwa kuhusika
na miili hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya madaktari wa IMTU.
Waandishi wakifuatilia tamko la Kamishna Kova
kuhusiana na tukio la viungo vya watu kukutwa eneo la Bunju.
|
Jeshi la
Polisi limesema litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya
kukamilika uchunguzi, jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa
hatua zaidi ili sheria ichukue mkondo wake.
Kamanda Kova
amewaomba wananchi kuwa watulivu na wasiwe na wasiwasi wakati upelelezi
ukiendelea.
(PICHA /
HABARI: MAKONGORO OGING', HARUNI SANCHAWA NA GABRIEL NG'OSHA / GPL)
No comments:
Post a Comment