Baada
ya safari ndefu ya Mwezi mzima iliyoanzia Juni 12,2014, hapo Jumapili Julai
13,2014,Fainali za Kombe la Dunia Nchini Brazil zitafikia tamati huko Estadio
Maracana, Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil, kwa Mechi ya Fainali ya Kombe la
Dunia kati ya Germany na Argentina.
Germany
imetinga Fainali hii kwa kishindo kikubwa kilichotikisa Dunia baada ya
kuwabwaga Wenyeji wa Mashindano Brazil Jumanne iliyopita kwa kipondo cha Bao
7-1 huku wakifunga Bao zao 5 za kwanza ndani ya Dakika 29 na Bao lao la Pili
hadi la 5 yakipigwa ndani ya kipindi cha Dakika 6 tu.
Argentina
walipata msukosuko kwenye Nusu Fainali yao na Netherlands kwa kwenda Dakika 120
wakiwa Sare 0-0 na hatimae kufuzu kwa Mikwaju ya Penati 4-2 hapo Jumatano.
Fainali
hii ya Jumapili inakumbushia Fainali za Miaka ya 1986 na 1990 miamba hii
ilipopambana.
Fainali
hizo ndizo mara ya mwisho kwa Nchi hizo kutwaa Kombe la Dunia wakati Argentina
ilipoifunga West Germany huko Mexico Mwaka 1986 na Germany kuifunga Argentina
Mwaka 1990 na kuwa Mabingwa wa Dunia.
Tangu
wakati huo, Argentina na Germany hazijatwaa tena Kombe la Dunia.
|
No comments:
Post a Comment