|
Mtoto Devota
Malole aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro, kufuatia mama
yake kumtesa kwa kumfungia ndani na kumlaza chini kwa muda wa miaka mitano
amehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya afya yake
kiafya kubadilika.
Mganga mkuu
wa hospitali ya wilaya ya kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema wamelazimika
kumuhamishia mtoto huyo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya
hali yake kuwa mbaya na uchunguzi wa awali umebaini anamagonjwa mbalimbali
ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika hospitali ya mkoa wa morogoro
waandishiwetu wameshuhudia madaktari wakifanya kila juhudi za vipimo na
matibabu.
Wasamaria
wema wamejitokeza katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia hali mtoto
Devota ambapo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood amewataka maafisa
ustawi wa jamii kuacha kulala na badala yake watekeleze wajibu wao ipasavyo
kuwasaidia watoto wanaoteseka.
Nae mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya Alsaidi,
Omari Alsaidy ameahidi kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata kama italazimika
kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.
|
No comments:
Post a Comment