![]() |
|
Moja ya
ndege ya PrecisionAir uwanjani. Picha Na:- Maktaba … Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kwenda Nairobi
nchini Kenya kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
|
Ndege ya
Shirika la PrecisionAir iliyokuwa imeruka kwa safari zake kutoka Mwanza kwenda
Nairobi nchini Kenya kupitia Kilimanjaro Julai 11,2014, imelazimika kutua kwa
dharura baada ya kupata hitilafu ikiwa angani.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege hiyo
namba 5H-PWC ATR 72, zilieleza kuwa tayari walikuwa wameruka lakini baada ya
muda mfupi waliambiwa hawawezi kuendelea na safari kutokana na ndege kupata
hitilafu.
Baada ya
kuruka, ndege ilitaka kukunja magurudumu kwa ndani ikashindikana hali
iliyomlazimisha rubani kuzunguka eneo la uwanja huo, huku akijaribu kuyarudisha
bila mafanikio na kuamua kutua kwa dharura.
Alisema
abiria 48 waliokuwa kwenye ndege hiyo walikuwa wanasubiri nyingine ili
kuendelea na safari.
Akizungumza
kwa simu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Ester Madale alisema hitilafu
hiyo ilikuwa ya kawaida hivyo haikuwa na madhara.
Madale
alisema iliruka saa 7:54 mchana kwenda Kilimanjaro, lakini baada ya kuruka
magurudumu yalishindwa kujikunja kurudi ndani hivyo rubani alijaribu
kuyarudisha ikashindikana, hivyo akalazimika kutua kwa dharura.
“Hitilafu
hiyo ni ya kawaida, wahandisi wetu waliangalia hitilafu hiyo na saa 9:15
alasiri walifanya majaribio kuirusha na imetua, hivyo siyo tatizo kubwa la
kawaida,” alisema Madale.
Matukio
ya karibuni
Desemba 13, 2013 ndege ya PrecisionAir aina ya ATR 42-600 ilipasuka magurudumu
manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA, miongoni mwa abiria waliokuwa ni
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Julai 24,
2012 ndege ya shirika la PrecisionAir magurudumu yalipasuka wakati ikitua
Uwanja wa Ndege mkoani Kigoma.






No comments:
Post a Comment