Akizungumza
na Radio Kwizera, Daktari katika hospitali ya Murgwanza Dr Mbise Willison ambaye ndiye aliyempokea mwanamke
huyo amesema amempokea jana majira ya
saa 2 usiku huku akiwa anavuja damu na
kisu alichojichoma kikiwa bado kimenasa
katika sehemu ya chini ya kifua ambapo ndipo alijichoma.
Amesema
baada ya kumpokea mgonjwa huyo walifanikisha kukiondoa kisu
hicho na kugundua kuwa kimeathili sehemu
ya Ini
na damu zilivujia kwa ndani na kusema kuwa damu hizo walifanikisha kuziondoa na hali ya
mgonjwa inaendelea vizuri ikilinganishwa na ilivyokuwa jana kipindi analetwa
hospitalini hapo.
Kwa upande
wake Dada yake ,Bi Jiliani Joshua ambaye
anamuuguza mwanamke huyo amesema
kuwa mdogo wake anashi na mwanaye mmoja
na haishi na mumewe na katika
kufanya tukio hilo alijifungia chumbani kwake na kufungulia muziki mkubwa na hivyo kujichoma kisu hicho na ndipo
majirani walifika kumuokoa na kufanikiwa kumfikisha hospitali na kwamba taarifa za
tukio hilo alizipata kupitia kwa majirani kwani yeye anashi mbali na yeye.






No comments:
Post a Comment