Khamis Mcha
baada ya kufunga bao la pili Kwa Taifa Stars.
|
Leo Julai 20,2014,katika Uwanja
wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza
vibaya hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani (2015) nchini Morocco,
baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Msumbiji.
Katika mchezo huo, uliofanyika jioni ya leo, mabao ya Stars inayofundishwa na
Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’
aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.
Mcha tena akaifungia Stars
bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa
Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.
Msumbiji walikuwa wa kwanza
kupata bao dakika ya 48 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe
baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari huku goli lililowapatia
bao la kusawazisha dakika ya 89 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi
pia.
Kwa matokeo, hayo Taifa Stars sasa itajitaji ushindi wa ugenini ili kusonga
mbele, au sare ya kuanzia mabao 3-3, wakati wenyeji wanaweza kunufaika na sare
ya 1-1 au 0-0.
Ikiwa 2-2 tena, mshindi ataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Taifa Stars iliyofika hatua hii baada ya kuitoa Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2
ikishinda 1-0 nyumbani na sare ya 2-2 Harare, ikifanikiwa kuitoa Msumbiji
itapangwa katika Kundi C ambalo lina timu za Zambia, Cerpe Verde na Niger
zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo, kuwania tiketi ya Morocco mwakani.
Taifa Stars imekuwa ikinyanyaswa na Msumbiji miaka ya karibuni na mara mbili imewahi kutolewa na Mambas katika hatua za awali za AFCON.
Kuwania Fainali za Ghana
mwaka 2008, Stars ikiwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo ilifungwa 1-0 Dar
es Salaam katika mchezo wa mwisho wa kundi.
Kuwania Fainali za mwaka jana (2013) Afrika Kusini, Stars ikiwa chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen, ilitolewa kwa penalti 5-4 na Msumbiji baada ya sare ya jumla ya 2-2.
John Bocco
akimpongeza Khamis Mcha baada ya kufunga bao la kwanza.
|
Mbwana
Samatta alisababisha penalti iliyozaa bao la pili.
|
Mbali ya Mechi ya Taifa Stars
na Msumbiji, Jana(Julai 19,2014) zilichezwa Mechi 3 nyingine za Raundi hii ya
AFCON 2015 na Timu zote za Nyumbani kushinda 2-0 kila mmoja.
Uganda iliichapa Mautitania
2-0, Botsawana kuipiga Guinea-Bissau 0 na Sierra Leone kuiwasha Seychelles 2-0.
Mechi za Marudiano za Raundi
hii zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA/MATOKEO.
Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19,2014.
Uganda 2 – 0 Mauritania
Botswana 2 – 0 Guinea-Bissau
Sierra Leone 2 - 0
Seychelles
Jumapili Julai 20,2014.
Lesotho 1 – 0 Kenya
Tanzania 2 -2 Mozambique
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
MAKUNDI.
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra
Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi
Botswana/Guinea-Bissau
No comments:
Post a Comment