Shule ya
msingi Kyamate ina wanafunzi 315 wavulana 160 wasichana155
walio katika madarasa ya muda yaliyojengwa kwa miti na kukandikwa kwa
udongo kisha kuezekwa kwa bati.
|
Na:-Shaaban
Ndyamukama-Muleba.
Mbunge wa
jimbo la Muleba Kusini ,Profesa Anna Tibaijuka ameahidi kujenga madarasa
matatu katika shule ya msingi Katanda na Kyamate wilayani Muleba,mkoani
Kagera baada ya kukuta wanafunzi wa shule hizo wakisomea katika madarasa
yasiyo bora.
Profesa
Tibaijuka amesema hayo june 08,2014 wakati alipofanya ziara ya kutembelea shule
hizo na kukuta walimu wa shule hizo wanafundishia katika vyumba vya madarasa
vilivyo jengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo kisha kuezekwa kwa bati.
Amesema
kufuatia hali hiyo atajenga chumba cha elimu ya awali katika shule ya msingi
Katanda ambapo wanafunzi 70 wa darasa hilo wanakaa chini katika jengo ambalo
limejengwa kwa miti na udongo lakini ni dhaifu na hatari kwa maisha yao.
Amepongeza
walimu wa shule za msingi Kyamate kwa kufanya
kazi katika mazingira magumu na kupata ufanisi kitaaluma na
kuwapatia Sh.500, 000 baada ya shule hiyo kuwa ya 11 kiwilaya katika
ufaulu wa darasa la saba mwaka jana.
Amewahimiza
wananchi kuchangia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao hasa
mchanga mawe kokoto na wanawake kuchota maji ili ili kulinda hadhi ya
shule hiyo ambayo ilikuwa ya 11 kati ya shule 228 za wilaya ya
Muleba.
Mwalimu mkuu
wa shule ya msingi Kyamate Severin Angelo amesema shule hiyo
ina wanafunzi 315 wavulana 160 wasichana155 walio
katika madarasa ya muda yaliyojengwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo
kisha kuezekwa kwa bati.
Amesema kuwa
shule hiyo ilianza mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi wa darasa la
kwanza 43kati yao wavulana 25 na wasichana 18 na changamoto kubwa
ni kukosekana kwa vyoo ikihiyaji matundu 14 ya wanafunzi na mawili ya walimu.
Naye
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Katanda Suleima Abdalah amesema shule
yake inao wanafunzi 568 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba ikiwa na
wanafunzi wa elimu wa awali 70 ambapo ilifunguliwa mwaka 2004
Alisema
wanafunzi wa shule hiyo wanatumia madawati 70 tu wengine wakika achini
huku walimu saba wa shule hiyo wakitumia ofisi iliyojengwa na
serikali isiyokuwa na meza wala viti na madarasa ya mudani nguvu za jamii.
Aidha
amesema shule hiyo inahitaji vyoo vya wanafunzi matundu 15 na mawili ya
walimu ambapo wanafunzi wa kiume wanatumia matundu ya muda yaliyo katika hali
mbaya kimatumizi na wanafunzi wanatumia matundu yaliyojengwa na serikali .
No comments:
Post a Comment