UJIRANI MWEMA /SOKA:-Soma Matokeo ya mechi kati ya Kabanga FC na Ilabilo FC ya Burundi(June 01,2014)mchezo ukipigwa mjini Kabanga-Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 02, 2014

UJIRANI MWEMA /SOKA:-Soma Matokeo ya mechi kati ya Kabanga FC na Ilabilo FC ya Burundi(June 01,2014)mchezo ukipigwa mjini Kabanga-Tanzania.

Timu ya Kabanga FC ikiwa nyumbani kwenye uwanja wake,imekubali kuchapwa bao 3-1 na wageni wao Timu ya Ilabilo kutoka mkoa wa Muyinga nchini Burundi katika mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa uliopigwa June 01,2014 mjini Kabanga,wilayani Ngara mkoani Kagera…Picha Na:- Soud Saidr-Kabanga.


Katika mchezo huo ,Ilabilo walitangulia kuongoza kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika na baadae kipindi cha pili kilipoanza Kabanga FC wakasawazisha bao hilo lakini Kabanga FC walishindwa kuulinda ushindi wao wa bao 1-0 waliposafiri kwenda kucheza nao kwao nchini Burundi, kwani walijikuta wakipwaya na kuruhusu kufungwa magoli 2  na kumaliza mchezo dakika 90,Ilabilo FC 3 na Kabanga FC 1.

........Kikosi cha timu ya Kabanga Eleven Fighters/Kabanga FC…..

.........Kikosi cha timu ya Ilabilo FC toka Muinga nchini Burundi...

Baadhi ya Mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa kwenye uwanja wa Kabanga June 01,2014...na Kabanga FC kufungwa bao 3-1 na Ilabilo FC .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad