ARSENAL KUTWAA FA CUP 2014:-Mashabiki wake mjini Ngara washerehekea kwa soka kati ya timu ya Mertesacker dhidi ya Giroud kwenye Bonanza uwanja wa Posta ya zamani wilayani Ngara,mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 02, 2014

ARSENAL KUTWAA FA CUP 2014:-Mashabiki wake mjini Ngara washerehekea kwa soka kati ya timu ya Mertesacker dhidi ya Giroud kwenye Bonanza uwanja wa Posta ya zamani wilayani Ngara,mkoani Kagera.


Kikosi cha Mashabi wa Kutupwa wa Klabu ya Arsenal kutoka Ngara mjini wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa Bonanza la Kufurahia Arsenal kubeba Kombe la FA CUP ,lililofanyika June 01, 2014 katika uwanja wa Posta ya zamani mjini Ngara na Baadae sherehe kubwa na ya aina yake  katika Ukumbi wa Muruvyagira kuanzia saa Moja usiku.




Aron Ntagalo Meneja Mauzo wa Airtel wilaya ya Ngara nae alishiriki katika Bonanza hilo la Mashabiki  wa Arsenal June 01,2014 kwenye Viwanja vya Posta ya zamani Mjini Ngara.


Damian Godrid ambaye ni shabiki mkubwa na wakutupwa wa Arsenal  akitafakari mchezo wa Mashabiki hao katika kuadhimisha Arsenal kubeba kombe la FA kwenye Viwanja vya Posta ya zamani Mjini Ngara.

Hii ni timu ya Giroud ikiongozwa na Seleman Ally aka Mzanzibar,Seif Upupu,Niyo,Baruan  na wengineo


Kikosi cha timu ya Mertesacker ambacho kiliibuka wababe kwa kuwafunga wenzao bao 4-1 .


Hapa kwa pamoja  Mashabiki wa Klabu ya Arsenal mjini Ngara waliojigawa na kuunda timu ya Mertesacker  v/s Giroud wakiwa katika picha ya wote kabla ya kupambana katika mchezo wa soka kama sehemu ya tukio la kufurahia Arsenal kubeba FA CUP.


Katika Bonanza hilo Mashabiki hao wa Arsenal walijigawa na kupata timu ya Mertesacker iliyopambana dhidi ya Giroud ambapo timu ya Mertesacker iliibuka wababe kwa kuwafunga wenzao bao 4-1 kwa magoli ya Asante Gwihangwe,Onesmo Josia,John Peter na Alex huku timu ya Giroud goli lao likifungwa na Wiliam Nyanungu.

Utakumbuka kuwa Baada ya  kukaa Miaka 9 bila Kombe lolote, baada kutwaa FA CUP Mwaka 2005, May 17,2014 katika Uwanjani Wembley, Jijini London, Arsenal wakafanikiwa kubeba FA CUP walipotoka nyuma kwa Bao 2-0 ndani ya Dakika 8 za kwanza na kushinda 3-2 katika Dakika 120 za Gemu…kwa magoli ya Santi Cazorla Dakika ya 17,Laurent Koscielny 71 na Aaron Ramsey 109.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad