PICHA/MASHABIKI WA ARSENAL-NGARA 2014:-Tazama Yaliyojiri katika Bonanza la Mashabi wa Arsenal wilayani Ngara June 01,2014 –kufurahia Arsenal kutwaa FA CUP. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 02, 2014

PICHA/MASHABIKI WA ARSENAL-NGARA 2014:-Tazama Yaliyojiri katika Bonanza la Mashabi wa Arsenal wilayani Ngara June 01,2014 –kufurahia Arsenal kutwaa FA CUP.


Mashabiki wa Klabu Kongwe ya Arsenal toka Ngara mjini wilayani Ngara mkoani Kagera wameshiriki katika Bonanza la Kufurahi/kusherekea Ubingwa wa timu yao ya Arsenal kufanikiwa kubeba FA CUP  2013/2014 katika sherehe ya aina yake na haijawahi kutokea kwa Mashabiki wa timu zingine za Ligi kuu Uingereza/Ulaya iliyofanyika June 01,2014 katika Ukumbi wa Murvyagira mjini Ngara na kuhudhuriwa na Mashabiki wa Klabu hiyo pamoja na mashabiki wachache kutoka Klabu pinzani za Manchester United,Manchester City,Liverpool na Chelsea.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza la Mashabiki wa  Arsenal toka Ngara mjini Donatus Baltazar akiwakaribisha wageni mbalimbali walioalikwa kuungana na Mashabiki wa Klabu ya Arsenal  Kufurahi/kusherekea Ubingwa wa timu yao ya Arsenal kufanikiwa kubeba FA CUP  2013/2014 .


Picha juu na chini ni muonekano wa baadhi ya Mashabiki wa Klabu Kongwe ya Arsenal toka Ngara mjini wakifatilia kile kilichokuwa kinaendelea katika sherehe iliyofanyika June 01,2014 katika Ukumbi wa Murvyagira mjini Ngara.



Mashabiki wachache kutoka Klabu pinzani za Manchester United,Manchester City,Liverpool na Chelsea nao walialikwa pia.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza la Mashabiki wa Arsenal ,Donatus Baltazar akiendelea na utambulisho wa wageni mbalimbali waliohudhuria kusherekea Ubingwa wa timu ya Arsenal kufanikiwa kubeba FA CUP  2013/2014.


Kuoka kulia ni Mtangazaji Dotto J.Bahemu na Seif Omary Upupu kutoka kituo cha Radio cha Mjini Ngara -Radio Kwizera FM nao waliwakilisha hisia zao sambamba na Gilman Mtegoa katika  sherehe hiyo .

Baadhi ya Mashabiki wa Klabu Kongwe ya Arsenal toka Ngara mjini wakifatilia kile kilichokuwa kinaendelea katika sherehe iliyofanyika June 01,2014 katika Ukumbi wa Murvyagira mjini Ngara.


Meza kuu,ikiongozwa na mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM -UVCCM wilaya ya Ngara Fares Addy Mohamed (katikati) ,Mwenyekiti wa Kamati ya Bonanza Donatus Baltazar,Dick Sempiga ambaye Ni shabiki mkubwa wa klabu ya Man United na Mwenyeiki wa Vijana wa Arsenal.


Aron Ntagalo akiilelezea hadhira Hisotia fupi ya Kombe la FA na kusema kuwa wanafurahi sana kwa klabu yao ya Arsenal kubeba kombe hilo la 11 kwa klabu yao na hivyo kuandika Historia.


Mdau na Shabiki wa Chelsea Mtayoba akibadilishana mawazo na Focas wakati wa sherehe hiyo  iliyofanyika June 01,2014 katika Ukumbi wa Murvyagira mjini Ngara.


Seleman Ally aka Mzanzibar ,kocha wa Ngara Stars na Mashabiki wa Klabu Kongwe ya Arsenal takifurahia jambo wakati wa sherehe ya Mashabiki wa klabu hiyo kubeba kombe la FA.
....Utawapenda tu kwa raha zao ....Mashabiki  hao wa Arsenal wakafungua Shampen na kugonga Cheers kwa furahaa.....
....Damiani Godrid na Cheers kwa furahaa.....
Cheers .............
.......Furaha ilikuwa zaidi ya maeleza kwa Mashabiki hawa wa Arsenal.....
Mwl.Adof Gisuka na Baba Lenon nao hawakukosa hasa wakifurahi na wimbo wa Arsenal ...we are Champion........
Mdau Elisante kushoto ,nae kama kawa alikuwa sehemu ya kufurahia klabu yao ya Arsenal kutwaa FA CUP 2013/2014.
.....Nao walikuwepo.......kufurahi.....
Mzee Kidenke mwenye shati jeupe na shabiki wa Man United nae alihudhuria kuungana na Mashabiki wa Arsenal kufurahia ushindi wa Kutwaa FA CUP ,katika sherehe iliyofanyika June 01,2014 kwenye ukumbi wa Muruvyagira mjini Ngara



....Mashabiki hao wa Klabu ya Arsenal  na wageni waalikwa ambao ni Mashabiki wa Vilabu vya Chelsea,Man City,Man United na Liverpool wakielekea kupata Chakula....



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad